Ni muhimu sana kuzielewa vyema aina zote za mazoezi na faida zake. Ni kawaida kukuta mdada mwenye nia ya kutengeneza shepu yake, akifanya mazoezi ya aerobics peke yake na kutegemea kutengeneza umbo au shepu anayoitaka. Hiki ni kitu kisichowezekana, kutokana na ukweli kwamba, kutengeneza shepu kunahusisha kupunguza sehemu fulani za mwili, kuongeza sehemu zingine na kubakiza sehemu zingine kama zilivyo. Hii inahitaji kufanya mazoezi ya aina mbali mbali yakiwemo yale ya resistance (kunyanyua au kusukuma uzito).