Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kurejea kwa wachezaji wa mkopo wa Real Madrid, akiwemo Dani Ceballos, mwenye umri wa miaka 23, katika Arsenal, kunaweza kuongeza fursa ya kuweka dau kwa ajili ya kiungo wa safu ya mashambulizi wa Paris St-Germain Mfaransa Kylian Mbappe, mwenye umri wa miaka 20. (AS)
 
Kiungo wa kati wa Barcelona raia wa Croatia Ivan Rakitic, mwenye umri wa miaka 31, yuko tayari kwa "ofa" katika kipindi cha uhamisho wa wachezaji mwezi Januari, huku Manchester United na Juventus wakimfuatilia mchezaji huyo . (marca)
 
Southampton wanamtaka Erik Stoffelshaus, ambaye amekuwa akifanya kazi katika klabu za Schalke na Lokomotiv Moscow, awe mkurugenzi wao mpya wa mchezo ,huku Manchester United pia wakiwa na nia ya kumuajiri mkurugenzi huyo mwenye umri wa miaka 48 . (Sun)
 
Liverpool walivaa fulana maalum katika mechi yao dhidi ya Tottenham iliyokuwa na maandishi "Futuremakers" ili kuutangazia umma kuhusu azma ya mdhamini wao mkuu Global initiative ya kukabiliana na ukosefu wa usawa kwa kukiwezesha kizazi kijacho kujifunza, kupata rizki na ukuaji. (Liverpool Echo)
 
Mpiga picha mmoja anapanga kutuma ujumbe wa malipo kwa klabu ya Brescia kwa kumpasulia kamera yake baada ya mchezaji wa zamani wa safu ya mashambulizi wa Liverpool na Manchester Mario Balotelli, 29, kuipiga teke baada ya kukasirika alipoondolewa uwanjani na kuingizwa kwa mchezaji mwingine.(Sun)
 
Afisa mkuu mtendaji wa Manchester United Ed Woodward, amekubali kutoa Β£125m kubadilishana wachezaji wawili wa Bundesliga akiwemo kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen na mchezaji wa kimataifa wa Ujerumani Kai Havertz, 20, na mshambuliaji wa Bayern Munich Thomas Muller, 30. (Mirror)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…