Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Staa Shevchenko rekodi zake kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya alizofanya akitamba na vikosi vya Dynamo Kyiv, AC Milan na Chelsea. Bao lake la kwanza kwenye michuano hiyo alifunga kwenye mchezo ambao Dynamo Kyiv walichapwa 4-1 na Bayern Munich, Desemba 7, 1994. Licha ya kwamba alikuja kushinda taji hilo mwkaa 2003, Andriy Shevchenko msimu wake bora kabisa kwenye michuano hiyo ulikuwa wa 1998/99 na 2005/06 ambapo alifunga mabao manane akiwa na kikosi cha Dynamo Kyiv na mabao tisa akiwa na kikosi cha AC Milan mtawalia, ambapo mara zote hizo alifika kwenye hatua ya nusu fainali.
 
Zlatan Ibrahimovic (48)

Zlatan Ibrahimovic amezurura kwenye timu nyingi sana huko Ulaya akipita Ajax, Juventus, Inter, Barcelona, AC Milan, Paris Saint-Germain na Manchester United, ambako kote alizotumikia kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kwenye michuano hiyo, bao lake la kwanza alifunga wakati Ajax ilipoitandika Lyon 2-1, Septemba 17, 2002. Katika mchezo huo, Ibra alifunga mabao yote mawili katika mechi yake ya kwanza kabla ya kuja kufunga 46 mengine katika kipindi cha miaka 14 aliyotamba katika timu kibao za huko Ulaya kabla ya kutimkia Marekani. Mechi zake za mwisho katika michuano hiyo zilikuwa kwenye msimu wa 2016/17.
 
Thierry Henry (50)

Unamkumbuka Thierry Henry, yule Mfaransa aliyekuwa matata kabisa katika kuifanya Arsenal kuwa timu tishio huko kwenye Ligi Kuu England. Lakini, fowadi huyo alitamba pia kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati alipotesa kwenye vikosi vya Monaco, Arsenal na Barcelona na kufanikiwa kufunga mabao kibao. Bao lake la kwanza Henry kwenye michuano hiyo alifunga kwenye mechi ya ushindi wa mabao 4-0 iliyopata Monaco dhidi ya Bayer Leverkusen, Oktoba 1, 1997. Hata hivyo, Henry alishindwa kabisa kuvuka ile rekodi yake bora kabisa ya kufunga mabao saba kwa msimu mmoja kama alivyofanya akiwa na Monaco katika msimu wake wa kwanza kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya, 1997/98.
 
Ruud van Nistelrooy (56)

Straika wa Kidachi, Ruud van Nistelrooy alitamba kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati wake alipokuwa mchezaji. Kwenye michuano hiyo aliwakilisha timu za PSV Eindhoven, Manchester United na Real Madrid. Bao lake la kwanza kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya alifunga akiwa PSV, katika mchezo wa kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Kaiserslautern, Novemba 4, 1998. Staa Ruud van Nistelrooy alikuwa kinara wa mabao kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa misimu mitatu tofauti, kipindi hicho alipokuwa Man United 2001/02, 2002/03, 2004/05. Katika msimu wa 2002/03 ulikuwa bora kabisa kwake, akifunga mabao 12 katika mechi tisa tu.
 
Robert Lewandowski (56)

Kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, straika Robert Lewandowski ametamba akiwa na vikosi vya Borussia Dortmund na Bayern Munich. Staa huyo wa kimataifa wa Poland amekuwa moto kwa kufunga, ambapo bao lake la kwanza kwenye michuano hiyo ya Ulaya alifunga kwenye mechi ya kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Olympiacos, kipindi hicho akiwa Borussia Dortmund, Oktoba 19, 2011. Bado hajabeba ubingwa wa taji hilo, lakini Robert Lewandowski amekuwa kwenye rekodi ya kuwa mchezaji aliyefikisha mabao 50 kwa haraka katika michuano hiyo, huku bao hilo akifunga dhidi ya Benfica akiwa amecheza mechi 77.
 
Karim Benzema (60)

Straika Mfaransa Karim Benzema kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya ametamba akiwa na vikosi vya Lyon na Real Madrid. Kwenye michuano hiyo, Benzema alifunga bao lake la kwanza kwenye ushindi wa mabao 2-1 iliyopata Lyon dhidi ya Rosenborg, Desemba 6, 2005. Staa huyo amekuwa hapewi sana sifa anayostahili licha ya kubeba ubingwa wa michuano hiyo mara nne na kuingia kwenye rekodi tamu kabisa za Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kwenye michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Benzema amekuwa na rekodi nzuri ikiwa ni moja ya wachezaji muhimu kabisa waliyoifanya Real Madrid kutamba na kubeba mataji kwa kadri inavyotaka.
 
Raul (71)

Gwiji wa Real Madrid, Mhispaniola Raul kwenye mchakamchaka wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ametamba akiwa na kikosi hicho cha Bernabeu na kile cha Schalke 04 ya Ujerumani. Bao lake la kwanza Raul alifunga kwenye mechi ya ushindi wa mabao 6-1 ambapo Real Madrid ilipata dhidi ya Ferencvaros, Oktoba 18, 1995. Kwa miaka mingi, Raul alikuwa kinara wa wakati wote wa mabao kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya na mabao yake 71 kabla ya kuja kupigwa kikumbo na wakali wawili, Cristiano Ronaldo na Lionel Messi. Raul alifunga hat-trick kwenye mechi yake ya kwanza katika michuano hiyo na alifikisha idadi ya mabao yanayofikia tarakimu mbili kwenye msimu wa 1999/00 huku pia akibeba ubingwa mara tatu.
 
Cristiano Ronaldo (127)

Staa huyo wa Kireno amepita kwenye klabu za Manchester United, Real Madrid na Juventus katika nyakati zake za kutamba katika mikikimikiki hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Bao lake la kwanza kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, Ronaldo alifunga kwenye ushindi wa 7-1 iliyopata Man United dhidi ya AS Roma, Aprili 10, 2007.
 
giphy.gif
 
Back
Top Bottom