Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Unaambiwa hivi, kuna wachezaji hao itakuwa ngumu sana kubaki kwenye timu zao wakati dirisha hilo la uhamisho wa majira ya kiangazi litakapofunguliwa kutokana na sababu nyingi tofauti, ikiwamo nguvu ya pesa, kutafuta mataji na nafasi za kucheza kwenye vikosi vya kwanza.
 
Hata hivyo, hiyo si kesi kubwa. Kuna timu hizo zitateseka sana katika kuwabakiza mastaa wao kwenye vikosi wakati dirisha hili litakapofunguliwa na utamu wa jambo hilo ni timu hizo ni vigogo, Paris Saint-Germain, Arsenal, Manchester United, Bayern Munich, Juventus, Liverpool na Tottenham Hotspur kwa kuzitaja kwa uchache huku zikitajwa pia Real Madrid na Barcelona.
 
Straika Harry Kane umri unakimbia na kama Spurs watashindwa kumhakikishia nafasi ya kubeba ubingwa, basi huoni kama fowadi huyo ataendelea kubaki hapo hasa baada ya kuwekwa kwenye rada za wababe Barcelona, Bayern Munich na Real Madrid, PSG na Man United.
 
Paul Dybala anaweza kufikiria kuondoka Juventus, Spurs wakimhitaji na kama wakali hao wa Serie A wakimsajili Mbappe, ambaye wanataka akamrithi Cristiano Ronaldo, basi watamfanya Muargentina huyo kwenda mahali ambako atakuwa staa mkubwa na kuheshimika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…