Kauli ya Solskjaer imekuja siku chache baada ya Rashford kukosa penalti katika mchezo wa Ligi Kuu England ambao Man United ilishinda mabao 3-1 dhidi ya Norwich City.
Chelsea ilifanya mabadiliko ya wachezaji sita waliocheza mechi ya Jumamosi dhidi ya Burnley. Christian Pulisic, aliyefunga mabao matatu kwenye Uwanja Turf Moor, jana hakucheza kwa kiwango bora.
KIMFAACHO mtu chake unaambiwa. Barcelona wanatafuta Pauni 100 milioni za kuongezea kwenye bajeti yao ya usajili wao na wanachokifanya ni kupiga bei masupastaa wao kibao.
Ivan Rakitic, Arturo Vidal na Philippe Coutinho wanatajwa kuorodheshwa kwenye kundi hilo baada ya kocha Ernesto Valverde kuwaona ni wa ziada katika kikosi chake.
Mpango wa klabu hiyo ni kupata Pauni 107 milioni kabla ya kufika Juni 30 mwakani ili kuweka vizuri bajeti yao ya usajili, hivyo wanatafuta njia za kujiweka sawa kifedha.
Gazeti la Marca linadai kwamba mazungumzo baina ya Barcelona, mastaa wake na baadhi ya wanunuzi yameshaanza chinichini ili kufanya mpango huo kukamilika.
Rakitic ni moja ya majina makubwa yanayohusishwa na mpango wa kuondoka Nou Camp baada ya Mcroatia huyo kushindwa kupenya kwenye kikosi cha Valverde msimu huu.
Coutinho yupo Bayern Munich kwa mkopo na huenda akabaki huko huko kama watafikia kwenye makubaliano huku Barca ikiwa imenasa saini yake kwa Pauni 142 milioni, Januari 2018.
Arturo Vidal naye yupo kwenye orodha hiyo kutokana na kuonekana muda mwingi kuanzia benchi, huku panga hilo linaweza kuwapitia pia mastaa wengine akiwamo beki wa kati Samuel Umtiti,
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.