Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Juzi Ronaldo alipiga hat trick katika pambano la kufuzu michuano ya Euro 2020 na sasa amefikisha mabao 98 katika kikosi cha Ureno na kubakisha mabao mawili tu awe mchezaji wa pili katika historia kufikisha mabao 100 katika vikosi vya timu ya taifa.
 
Ureno imebakisha ushindi mmoja tu kufuzu michuano hiyo lakini alikuwa Ronaldo ndiye aliyeiteka shoo baada ya kufunga mabao hayo matatu na anaweza kufikisha mabao 100 kama atafunga mabao mawili dhidi ya Luxembourg Jumapili.
 
Katika pambano la juzi, Ronaldo ambaye ni nahodha wa timu yake hiyo ya taifa alifunga bao la mapema kwa penalti kabla ya kufunga jingine la pili nba baada ya hapo mastaa wenzake wa Ureno, Pizzi, Goncalo Paciencia na Bernardo Silva wakafunga bao moja moja kabla ya Ronaldo kukamilisha hat trick yake.
 
Hiyo inakuwa hat trick ya 55 kwa Ronaldo katika maisha yake yote ya soka ukijumlisha katika klabu alizopitia pamoja na timu yake ya taifa lakini kwa upande wa timu ya taifa pekee hiyo inakuwa hat trick yake ya tisa.
 
Ronaldo anaelekea kuzeeka na ubora wake kwa sababu hat trick saba katika ya tisa alizopiga akiwa na kikosi cha Ureno amefunga baada ya kupitisha umri wa miaka 30. Kwa sasa ana umri wa miaka 34 ingawa bado ana makali yake.
 
Mpaka sasa rekodi ya mchezaji aliyeifungia timu yake ya taifa mabao mengi zaidi inashikiliwa na mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa Iran, Ali Daei ambaye mpaka sasa amefunga mabao 109. Ronaldo amebakisha mabao 11 kumfikia Daei.
 
Mwaka huu Ronaldo ambaye ni staa wa zamani wa Sporting Lisbon, Manchester United na Real Madrid amefunga mabao 13 katika mechi saba tu alizocheza na amefikia rekodi yake ya kufunga mabao mengi ndani ya mwaka mmoja baada ya awali kufanya hivyo mwaka 2016.
 
Kuelekea katika pambano la juzi Ronaldo alikuwa ameingia katika mgogoro na kocha wake klabuni Juventus, Maurizio Sarri ambaye alimtoa nje kwa mechi mbili mfululizo na katika pambano la wikiendi iliyopita Sarri alidai Ronaldo alikuwa ana tatizo la goti
 
Hata hivyo, wachezaji wenzake wa kikosi cha timu ya taifa walidai Ronaldo alikuwa fiti na alikuwa katika mazoezi kama kawaida, huku baada ya mechi ya juzi, kocha wake katika kikosi cha timu ya taifa, Fernando Santos akidai Ronaldo alikuwa fiti kucheza mechi hiyo na hakuwa na shida yoyote.
 
Katika pambano jingine la kundi hilo la B Serbia iliichapa Luxembourg mabao 3-1 huku mabao mawili kati ya hayo yakifungwa na mshambuliaji wa Fulham, Aleksandar Mitrovic na hivyo kufanya mchezo wa timu ya pili ya kufuzu katika kundi hilo kwenda mpaka mwishoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…