Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

72616446_159305071940754_4341651493421490080_n.jpg
 
Mkoani Kilimanjaro (Uru), tajiri mmoja aliyeishi muda mwingi ughaibuni, aliomba kujenga vyumba vitatu vipya vya madarasa kwa masharti ya majengo hayo kutajwa kwa jina lake, alinyimwa fursa hiyo.
Mbali ya vyumba hivyo tajiri huyo aldhamiria kuikarabati shule yote pamoja na kuiwekea umeme, uzio, rangi nk, uongozi wa kijiji, kata na wilaya umemkatalia maombi yake hayo kwa shule hiyo ambayo yeye mwenyewe alisoma
Nilishawahi kuandika makala kuhusu huu utaratibu mzuri. Kwa wenzetu huko Marekani utakuta majengo mengi katika vyuo vikuu ni majina ya watu. Ukiulizia utaambiwa ni wanafunzi waliosoma hapo na sasa wamerudi kutoa shukrani kwa kutoa mamilioni ili majengo yajengwe na kupewa majina yao. Lengo ni kuendeleza legacy. Mtu anaweka akiba maisha yake yote ili siku ya siku naye atoe mchango wake hata kama ni chumba kimoja tu katika jengo la umma kipewe jina lake. Na majimbo mengi yana utaratibu wa kuoanisha kiasi sawa cha pesa. Yaani milionea akitoa dola milioni 10 kujenga jengo litakaloitwa SYB Institute of Economics jimbo nalo ni lazima litoe milioni 10. Matokeo yake linajengwa jengo kabambe la dola milioni 20. Utaratibu huu umewasaidia sana kuwa na vyuo vikuu vikubwa, imara na vya kisasa. Siyo sisi kila tajiri na fisadi anawaza tu kuficha pesa zake...
 
Back
Top Bottom