Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

"Kwa wenzetu huko marekani"[emoji3526][emoji3526].
Nakusalimu msukuma[emoji137]
 
Licha ya kuwa mmoja kati ya washambuliaji bora duniani kwa muda mrefu, Benzema hajaitwa katika kikosi cha Ufaransa kwa muda mrefu kutokana na kesi iliyomkabili dhidi ya staa mwenzake wa zamani wa kikosi cha Ufaransa, Mathieu Valbuena
Ilidaiwa Benzema pamoja na kundi la marafiki zake wasiokuwa wanasoka walimwambie Valbuena awape pesa ili wasiusambaze mkanda wa ngono wa nyota huyo ambao walidai wameutia mikononi mwao na kuanzia hapo Kocha wa Ufaransa, Didier Deschamps amekuwa akimuacha Benzema katika kikosi cha timu ya taifa.
 
Benzema alikosa michuano ya Euro 2016 iliyofanyika kwao Ufaransa lakini pia akakosa katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 ambapo Ufaransa ilitwaa taji hilo. Na sasa ametumia mtandao wake wa kijamii kudai anafikiria kwenda kucheza taifa jingine ikiwa ni jibu lake baada ya kukerwa na kauli iliyotolewa na Rais wa Shirikisho la Soka la Ufaransa, Noel Le Graet hivi karibuni.
 
Noel, nilidhani haufanyi kazi ya kuingilia maamuzi ya makocha. Nataka ujue ni mimi mwenyewe tu ndiye ambaye ninaweza kumaliza maisha yangu ya soka la kimataifa. Kama unadhani nimeisha acha nicheze katika moja kati ya nchi ambazo naruhusiwa kuchezea na tutaona,” aliandika Benzema.
 
Karim Benzema ni mchezaji mzuri sana. Sijawahi kuwa na wasiwasi na ubora wake. Kinyume chake anaonyesha pale Real Madrid ni mmoja kati ya wachezaji bora dunini. Hata hivyo, suala lake na timu ya taifa limefika mwisho,” alisema Le Graet.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…