Samuel Eto’o – Inter/Chelsea
Fowadi mwenye heshima yake huko Cameroon, Samuel Eto’o ni mwanasoka mwingine maarufu wa Kiafrika kuwahi kuwa chini ya Mourinho katika maisha yake ya soka. Kwanza, Mourinho na Eto’o walikutana huko Inter Milan na kufanya kazi nzuri pamoja, wakibabe mataji matatu ndani ya msimu mmoja mwaka 2010. Lakini, badaaye, wakati Mourinho aliporejea Chelsea kwa mara ya pili, alimnasa tena Eto’o na kuwa chini yake huko Stamford Bridge. Rekodi zinaonyesha kwamba chini yake Mourinho, Eto’o alicheza mechi 83 na kufunga mabao 28.