Mastaa wengine wa Kiafrika
Mourinho hana shida na wanasoka wa Kiafrika, akiwa amefanya kazi na mastaa wengi sana na kupata mafanikio pamoja. Miongoni mwa mastaa hao ni staa wa zamani wa Cameroon, Geremi Njitap, ambaye alikuwa naye pamoja huko Chelsea, akicheza mechi 69 chini yake na kufunga mabao matatu, huku kwenye kikosi hicho cha Stamford Bridge alimnoa pia Mnigeria, Victor Moyes, akicheza mechi moja tu chini yake kabla ya kumtoa kwa mikopo mara kadhaa. Staa mwingine wa Afrika kuwa chini ya Mourinho ni beki wa kati, Eric Bailly, ambaye ndiye aliyekuwa mchezaji wa kwanza kumsajili baada ya kubamba ajira ya kuinoa Manchester United.