Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Sheikh Karume yeye alikuwa hawezi kufanya lolote bila ya kuzungumza na Mwalimu Nyerere na kama itavyoamuliwa na Mwalimu, ndivyo hivyo hivyo atavyofuata hata ikiwa si maslahi kwa Zanzibar (na mara nyingi hivyo ndivyo ilivyokuwa). Sheikh Mohammed Shamte, hayo yeye alikuwa hayakubali; kwahivyo daima walikuwa wakibuburushana mpaka mambo yalipofika hadi ya kufanywa mikutano ya Kamati Kuu ya Chama bila ya kuarifiwa Sheikh Mohammed kwa kukhofiwa kuwa akiwepo ataleta upingaji juu ya baadhi ya mambo. Ilipofika kiwango hichi, maji kuzidi unga, Sheikh Mohammed na Sheikh Ali Shariff walijitoa katika AfroShirazi.
 
KUASISIWA KWA ZANZIBAR AND PEMBA PEOPLES' PARTY (ZPPP) Chama cha Z.P.P.P. kiliasisiwa Novemba, 1959. Raisi wa Chama alikuwa Sheikh Mohammed Shamte Hamad na Naibu Raisi alikuwa Sheikh Ameir Tajo. Makao Makuu ya Chama yalikuwa Malindi Zanzibar. Z.P.P.P. kilikuwa Chama cha wananchi wa Unguja na Pemba. Kwa Unguja hakikuweza kupata wanachama wengi kwa wakati huo lakini kwa Pemba kiliweza kupata wananchi wengi kujiunga katika chama. Misingi na dhamiri ya Z.P.P.P. ikilingana na ya HizbulWattan. Nayo ni kufanyakazi kwa pamoja Wazanzibari wote, bila ya kubali rangi, kabila au imani zao za kidini katika kugombania kupatikana Uhuru wa Zanzibar kwa ajili ya mslahi ya wananchi wote. Waongozi wa HizbulWattan hawakuwa na shaka yoyote juu ya uzalendo wa Sheikh Muhammed Shamte na wenziwe, kwahivyo walikuwa wakiamini kuwa iko siku wataweza kufanyakazi pamoja.
 
TUME YA SIR HILLARY BLOOD
Katika Mei, 1960 Serikali ya Kiingereza baada ya juhudi kubwa zilizokuwa zikifanywa na Chama cha Hizbu juu ya kutaka yapatikane maendeleo zaidi juu ya mabadiliko ya Katiba katika nchi, walimleta Sir Hillary Blood kutoka Uingereza akiwa ni mchunguzi wa mabadiliko ya Katiba. (Huyu ni wa pili, wa kwanza alikuwa Mr. Coutts). Hizbu kama kawaida yao waliandaa maandamano makubwa kutoka kiwanja cha ndege cha Kiembe Samaki mpaka mbele ya nyumba ya Balozi wa Kiingereza. Waandamanaji wote wa kike na wa kiume, walichukuwa mabango yaliyoandikwa neno moja tu, "UHURU 1960".
 
Sir Hillary Blood alipofika Zanzibar alivikuta vyama vitatu vya siasa, Zanzibar Nationalist Party (ZNP) yaani HizbulWattan, AfroShirazi Party yaani A.S.P. na Zanzibar and Pemba Peoples' Party yaani Z.P.P.P. Vyama vyote vitatu vilimpelekea Sir Hillary Blood risala za matakwa yao na vilevile Sir Hillary alipokea risala kutoka katika vyama vya wafanyakazi na kutoka kwa watu binafsi.

Pia alizungumza na kuchukua fikra na nasaha kutoka kwa watu mbali mbali. Risala ya Hizbu na risala ya Z.P.P.P. zililingana sana katika matakwa yao. Zote mbili zilitaka Wawakilishi wote wa Baraza la Kutunga Sheria wawe wananchi waliyochaguliwa katika uchaguzi wa "One Man One Vote". Na baada ya matokeo ya uchaguzi huo yafuatiye mazungumzo ya Uhuru kamili wa Zanzibar. Ama risala ya AfroShirazi Party, ilitaka Wawakilishi wote wa Baraza la Kutunga Sheria wawe 25 na katika hao 22 wawe ndio wa kuchaguliwa kwa njia ya uchaguzi na watatu waliyobakia wawe miongoni mwa wafanyakazi wa Serikali ya Kiingereza waliopo nchini, hawa wateuliwe na Balozi wa Kiingereza.
 
Kwa faida ya wasomaji, nitazinukulu sehemu muhimu za risala zote tatu, yaani ya Hizbu, ya AfroShirazi na ya ZPPP. Kwa kufanya hivyo hapana shaka itakuwa faida zaidi kwa wananchi na khasa kwa vichipukizi vyetu, na wao wapate kujionea kwa macho yao, chama gani kilichokuwa kikiwakumbatia na kuwataka wakoloni waendelee katika uwongozi wa Serikali ya Zanzibar. Pia wapate vilevile kujionea wenyewe vyama gani vilivyokuwa vikitaka upatikane Uhuru kamili wa nchi.
 
Risala ya Hizbu ilikuwa kama hivi: ".....
.It is unnecessary now to argue whether or not it is our right to rule ourselves completely and whether or not we have the capacity to do so.
Those days are over. There are now no two sides to the question. ".......

In framing the recommendations regard should be paid to Her Majesty's Government's view that the legislature should become predominantly elective in character and that the executive should be reorganized to permit the establishment of a ministerial system. "

......Under any circumstances, you will be failing in your duty and mocking the people of Zanzibar if you recommend anything less than full independence for the country".
 
Risala ya Z.P.P.P. ilikuwa kama hivi:
".....That the Zanzibar and Pemba Peoples' Party feels that this Sultanate should be given full independence within the British Commonwealth soon after the next election.

"....That the Legislative Council should be of 30 members and that all 30 seats should be contested on Common Roll Election as stipulated in your terms of reference".
 
Risala ya AfroShirazi Party ilikuwa kama hivi:

".......the AfroShirazi Party believes and recommends that the Legislative Assembly should consist of no more than 25 seats of which three seats should be reserved for Ex-Officio members. The rest should all be open seats to be fought in Common Roll Election. "

......The Ex-Officio members should be the Minister for Justice, Minister of Finance and Minister of Defence and External Affairs. "

......It will indeed be befitting, and we entreat Her Majesty's Government, that 30th October 1960, should mark the granting of self-government to the people of these islands".
 
Mimi sitoongeza langu ila ninawaachia wasomaji baada ya kuzisoma risala zote tatu waamuwe wenyewe, ni wepi hao waliyokuwa bado wakitaka kurambatia urojo wa wakoloni. Ikiwa Wizara ya Uadilifu, Wizara ya Fedha na Wizara ya Ulinzi na Mambo ya Nje, ziwe katika mikono ya wakoloni, sasa wananchi watakuwa wamejitawala kitu gani? Ndio wenye kuitambua siasa ya AfroShirazi, na kwa kujidhihirisha zaidi kwa kimaandishi kama hivi, hawakustaajabu walipomuona Karume ameyatia mambo yote muhimu kwa nchi, chini ya amri ya Serikali ya Muungano ambayo kwa ukweli ni Serikali ya Tanganyika, chini ya amri ya ya Bwana Nyerere.
 
Umoja wa Vijana wa Youth Own Union walikasirishwa sana na mapendekezo ya Sir Hillary Blood. Kwa kuthibitisha uchukivu wao, waliandaa mkutano maalumu wa hadhara katika mtaa wa Mwembe Sanda, Miembeni, mkutano huo ulihudhuriwa na mamia ya wananchi.

Baada ya kusomwa mapendekezo ya 19 Mchunguzi huyo mbele ya wananchi, ilikubaliwa kuilani na kuichoma moto ripoti hiyo, kwa vile ilivyo kwenda sana katika kudharau matakwa ya wananchi. Pia ilikubaliwa katika mkutano huo kumpelekea Sir Hillary risala maalumu kutoka kwa Umoja wa Vijana wa Youth Own Union ya kupinga mapendekezo yake aliyoyatoa kukhusu maendeleo ya Katiba katika Zanzibar.
 
Mapendekezo aliyoyatoa Sir Hillary Blood katika uchunguzi wake ni kuwa viti 22 tu viwe vya kuchaguliwa katika uchaguzi wa "Common Roll Election" na viti vinane viendelee kuwa vya kuteuliwa na Balozi wa Kiingereza kwa kushauriana na Mfalme wa nchi, yaani vyote viwe 30. Mapendekezo yake haya hayakuwa mbali na yale ya Chama cha AfroShirazi. Kama tulivyoona hapo juu katika risala yao, AfroShirazi wao walipendekeza kuwa viti vyote visizidi 25, kati ya hivyo vitatu viwe vya wajumbe wa kuteuliwa na kuchukuwa nafasi muhimu katika serikali.
 
UCHAGUZI WA PILI, JANUARI 1961
Baada ya miaka mitatu unusu tokea kufanyika kwa uchaguzi wa mara ya mwanzo, Juni 1957, ulifanywa uchaguzi mwengine, katika Januari, 1961. Safari hii, mabibi nao walipata fursa ya kushiriki katika uchaguzi. Uchaguzi huu ulikuwa wa viti 22. Vyama vyote vitatu vilishiriki kwa ukamilifu. Matokeo ya uchaguzi huo yalikuwa, AfroShirazi walipata viti 10, Hizbu viti tisa na ZPPP viti vitatu.

Kwa natija hii, hapakuwa na chama kilichoweza kuunda Serikali ila kwa kushirikiana na chama chengine. Balozi wa Kiingereza Sir George Mooring aliwaalika waongozi wa vyama viwili vikubwa, yaani Hizbu na AfroShirazi kwa kuzungumzia tatizo liliokuwepo juu ya utaratibu wa kuweza kuunda serikali. Baada ya mazungumzo marefu ya hivi na hivi mwongozi wa Chama cha Hizbu, Sheikh Ali Muhsin alitoa shauri la kutaka ifanywe serikali ya pamoja ya vyama vyote vitatu. Mwongozi wa Chama cha AfroShirazi, Sheikh Abeid Amani Karume, yeye aliipinga shauri hiyo na badala yake alitaka matokeo ya uchaguzi huo yafutwe na pafanywe uchaguzi mwengine.
 
Baada ya kuzozana zozana na pasipatikane natija yoyote ya kurahisisha tatizo hilo, Balozi wa Kiingereza, Sir George Mooring alimpa kila kiongozi katika hao wawili muda wa wiki moja ajaribu kupata waakilishi waliyochaguliwa kuchanganya viti vyao pamoja naye ili aweze kupata wingi wa viti vya kumuwezesha kuunda serikali. Fursa hiyo kwanza alipewa Sheikh Abeid Amani Karume kwa kuwa Chama chake kilipata kiti kimoja zaidi kuliko Chama cha Hizbu.
 
Wakati Karume alipokuwa katika juhudi za kuzungumza na Chama cha ZPPP, kwa kuwataka waviunge viti vyao vitatu upande wa Chama cha AfroShirazi, baadhi ya watumishi wa Serikali wa kikoloni na khasa wa Idara ya Utawala, nao waliingia kazini kwa kufunga njuga kwa njia za siri siri. Miongoni mwa utumishi wao ilikuwa ni kukisaidia Chama cha Afro waweze kupata viti vya kutosha waunde serikali. Kwa kutaka kutekeleza utumishi wao huo walizungumza na Sheikh Othman Shariff na walimtaka afanye kila njia na kila jitihada mpaka ampate Sheikh Mohammed Shamte akubali kuvipeleka viti vyao (vya ZPPP) vitatu upande wa AfroShirazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…