Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

😀😀😀
nimemkumbuka member fulani humu ndani jina namuhifadhi, alikuja mahakamani kunifungulia mashitaka
basi tokea siku hiyo nikaacha kumtania matani yaleeeee asiyoyapenda.
Yeah!

Mtu akisema hataki matani fulani ni lazima kutii matakwa yake vinginevyo utakuwa unamkwaza.

Nimejitahidi kusoma hiyo historia ya Zanzibar unayoshusha. Mzee Mohamed Said kuna thread huko anasema historia ya Visiwani inayofundishwa mashuleni imepotoshwa sana na kuna haja ya kuinyoosha. Natumaini hii yako ni ile iliyonyooshwa.
 
unnamed%20(4).jpeg
 
Yeah!

Mtu akisema hataki matani fulani ni lazima kutii matakwa yake vinginevyo utakuwa unamkwaza.

Nimejitahidi kusoma hiyo historia ya Zanzibar unayoshusha. Mzee Mohamed Said kuna thread huko anasema historia ya Visiwani inayofundishwa mashuleni imepotoshwa sana na kuna haja ya kuinyoosha. Natumaini hii yako ni ile iliyonyooshwa.
historia ya mapinduzi kila upande unaandika kivyake kwa lengo la kutaka waonekane ni malaika.
waliopinduliwa hawawezi kuyasifu mapinduzi
waliopindua hawawezi kusifu utawala wa sultani.

hiki kitabu ameandika marehemu amani thani mmoja kati ya wafungwa wa kisiasa na pia kiongozi wa zamani wa ZNP
 
KUFUNGWA GEREZANI KWA ABDULRAHMAN BABU

Serikali ya kikoloni ilikuwa daima dawamu dhidi ya misingi na msimamo wa Chama cha Hizbu, haikutokea hata mara moja kukipa uso mzuri. Kwa vile hawakupendelea kiendelee, kila wakati walikuwa wakikitafutia kila njia ya kukivuruga ili kisiweze kuwa na nguvu, na ikiyumkinika hata kitoweke kabisa. Lakini kila wakizidisha njama zao ndio umma ukizidi kuwafahamu na jitihada zao zikifeli.
 
Babu wakati huo alikuwa ni miongoni mwa waliyokuwa hawapendiza machoni mwa wakoloni, kwa hivyo naye pia alikuwa katika mipango ya njama zao. Walipopata kipengee kutokana na makala aliyoyaandika katika gazeti lake la ZANEWS, wakoloni waliona sasa mtego wao umeweza kumnasa Babu. Pia waliona kuwa natija yake itafaa kutumika dhidi ya Hizbu.

Wakoloni walimshitaki Babu kwa kosa la kuwa makala yake ni matusi ya kumtukana Mkuu wa Polisi kwa jambo la uwongo wala si kwa maslahi ya umma. Kamati Kuu ya Hizbu bali hata wananchi wengi ilifahamu wazi kuwa wakoloni wamechukua khatua hiyo ya kumshitaki Babu si kwa sababu yoyote illa ni kutaka kukidhoofisha Chama katika wakati muhimu kama huo katika juhudi za ugombozi wa nchi kutokana na ukoloni.
 
Kamati Kuu ya Hizbu iliamua kushirikiana na Babu katika kesi hiyo kwa hali na kwa mali, juu ya kuwa gazeti hilo la ZANEWS halikuwa gazeti la Chama bali lilikuwa la Babu binafsi. Gazeti hilo likilipiwa na Shirika la Kichina liitwalo "Hsinhua Chinese News Agency". Kutokana na mipango yake, Babu aliweza kupata wakili kutoka Uingereza aliyejitolea kumsimamia katika kesi hiyo bila ya kuchukua malipo.
 
Wakili huyo alitaka basi alipiwe ukaaji wake katika hoteli kwa muda wa siku atazokuwepo nchini na matumizi madogo madogo. Bibi Azza Mohammed (mamewatoto wa Sheikh Ali Muhsin) alijitolea kwa niaba ya Hizbu kuzilipa gharama zote hizo. Kwa vile wakoloni walikuwa wamekwisha dhamiria kuitumia fursa hii kwa azma ya kuleta michafuko katika Chama, walitekeleza azma yao kwa kumfunga Babu gerezani kifungo cha miezi 18.

Chama kilikata rufaani kwa hapo Zanzibar na baada ya kushindwa hapo, kilichukua rufaani kutoka "East African Court of Appeal" na huko pia kilishindwa na Babu aliendelea na kifungo chake kwa muda wa miezi 18, kama ilivyokwisha pangwa.
 
Back
Top Bottom