D A E M U S H I N
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 22,665
- 121,102
UHURU WA ZANZIBAR
Manamo saa sita na dakika moja za usiku wa kuamkia taarikhi 10 Disemba 1963, bendera nyekundu tupu iliteremshwa kutoka kwenye mlingoti wake na Bendera ya Dola Huru ya Zanzibar yenye karafuu mbili ilipandishwa na kupepea katika mlingoti uliokuwepo kwenye ardhi ya nchi katika uwanja wa Mivinjeni (Coopers Insititute), uwanja huo hivi sasa ati unaitwa "Uwanja wa Maisara".
Tafauti na koloni nyengine za Muingereza, Zanzibar haikuwepo bendera ya Kiingereza kuteremshwa, kwa sababu haikupatapo kupepea juu ya ardhi ya Zanzibar. Japokuwa ilitiwa chini ya himaya ya Kiingereza, haikuwa koloni kama vile koloni nyenginezo za Kiingereza, Zanzibar haikusita kuwa Dola kwa muda wote huo.