Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

UCHAGUZI WA MWANZO JUNI 1957
Kutokana na mapendekezo ya uchunguzi wa Bwana Coutts kukhusu uchaguzi, uchaguzi wa mwanzo ulifanyika, June, 1957. Na kwa uchaguzi huo ndio wananchi wa Unguja na Pemba kwa mara ya kwanza waliweza kushiriki katika kuwachagua Wawakilishi wao wa Baraza la Kutunga Sheria la nchi yao. Uchaguzi huu ulikuwa wa viti sita. Majimbo mane yalikuwa kwa Unguja na mawili Pemba.

Majimbo sita hayo yaligaiwa kama hivi:
Unguja: Majumba ya Mawe
Unguja: N'gambo
Unguja: Kaskazini Unguja:
Kusini Pemba:
Kaskazini Pemba: Kusini
Sawasawa
 
KIPI KILICHO MPELEKEA BABU KUCHUKUA KHATUA KAMA HIZO
Kama nilivyotangulia kusema, Babu alikuwa na dhamiri zake ambazo alifikiria ataweza kuzitekeleza kwa kukitumilia Chama. Alipoona kuwa kila alilojaribu kulileta, halikuweza kufuzu, ndipo alipochukua khatua kama hizo na katika wakati kama huo. Babu alikhadaika kwa maneno aliyokuwa akiambiwa na hao wafuasi wake wajiitao "progressives" wakati alipokuwepo kifungoni.

Maneno waliyokuwa wakimpelekea baada ya wao kuwa wakipita wakitangaza propaganda dhidi ya uwongozi wa Hizbu, ni kuwa, "Umma wote wa Hizbu upo nyuma yako na kama utavyoamua baada ya kutoka kifungoni, ndivyo na wao watavyofuata. Ukiamua kutoka katika Chama, basi Umma utakufuata na ukiamua kubakia, nao utabakia na wewe".
@Daemusin sunbaenim ahsante sana [emoji122][emoji122][emoji122] sikutegemea utafurahi mapema kiasi hiki
 
KIFO CHA ALI MZEE MBALIA
Binaadamu kujidhulumu maisha yake mwenyewe kwa njia yoyote ni katika makosa makubwa mbele ya Mwenyezi Mungu, lakini Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa yote ya dhaahiri na ya siri. Tunmweomba Mwenyezi Mungu na tunatumai kuwa atatupokelea maombi yetu na kumsamehe kiumbe chake hiki kwa makosa aliyo lazimika kuyafanya ya kujidhulumu nafsi yake. Kutokana na mateso aliyo kuwa ameyapata kijana huyu, Ali Mzee Mbalia, alipo kuwepo katika gereza la "Kwa Ba Mkwe" (Mlango wa nyuma) aliamua kufa kuliko kuishi katika mateso. Ali Mzee alikuwa kijana mdogo mwenye kupendeza kwa sura na kwa umbile lake.

Alikuwa akipendana na kijana mwenziwe wa kike na walikuwa wamesha ahadiana kuoana. Wakati wenyewe walipokuwa wakiyapanga hayo, huku 34 pembeni alitokea Mheshimiwa Mkuu wa Jeshi la Zanzibar, Brigadiya. Kwa bahati mbaya Mheshimiwa "alifol", hajijui hajitambui, kwa hicho kijitoto cha kike. Msichana huyo alikuwa hakuathirika naye, kwani alikuwa akiliona hilo ni Baba Zere tu kwake
 
Brigadiya alipogundua kuwa msichana anapendana na kijana mwenziwe, naye anamfanya yeye ni mpumbavu, dashere tu, alimnyakua Ali Mzee mpaka Mlango wa Nyuma kwa Ziraili Mandera, na huko aliwapa amri wamtese kijana huyo kila mateso mabaya waliyo fundishwa, na waliyo yazua wenyewe.
 
IMG-20191201-WA0002.jpeg
 
Ali Mzee aliteswa mateso mabaya sana hata si vizuri wala si heshima kuyataja katika maandishi. Kutokana na mateso hayo aliyo kuwa akiyapata, alitokewa na kila namna ya maradhi, na aliachwa humo humo gerezani akiteseka. Hali ilipokuwa mbaya sana, alipelekwa hospitali kuu Mnazi Mmoja na baada ya kutibiwa kwa muda, alipata afuweni, na alianza kutembea tembea kwa miguu yake.

Siku Daktari alipo mwambia kuwa kesho atapata ruhusa, na ruhusa yenyewe ni kurejeshwa gerezani kwa Ba Mkwe, ndipo alipoazimia bora afe kwa kujitupa kutoka ghorofa ya tatu ya hospitali mpaka chini. Huo ndio ulikuwa mwisho wa maisha yake. Kwa maafa hayo yaliyo mtokea Ali Mzee, kijana wa kike ndio alizidi kuchongeka ukali na kutomkubali Brigadiya kabisa. Hayo ndiyo yaliyo kuwa yakifanywa na wakuu wengi wa serikali ya mavamizi, khasa katika Awamu ya Mwanzo
 
Back
Top Bottom