Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Nilipofika nyumbani, nilikuta nyumba imejaa watu kwani khabari za kutolewa kwetu gerezani, zilienea mji mzima. Vilio vya furaha vilianikiza majumbani mwetu na kila dakika hawa wakiingia na hawa wakitoka kwa furaha na bashasha. Kwa upande wetu siku hiyo ilikuwa siku kubwa sana kwa mengi bali, khasa kwa haya, la kwanza ni kwa kurejeshewa uhuru wa nafsi zetu, uhuru ambao tulinyang'anywa kwa muda wa siku 1095 yaani miaka mitatu na kitu tukiwa wafungwa wa Nyerere na Karume.
 
NAKIMBILIA DARESSALAAM
Kutokana na hali kama hizo zilizokuwepo nchini, namiye niliamua kuikimbia nchi yangu. Taarikhi 10 Juni, 1967 niliondoka Zanzibar kwa kuhamia DaresSalaam na huko nilifikia, na nilipokelewa na ndugu yangu mpenzi Mzee Mohammed MBABA. Tuliishi pamoja kwa muda mkubwa na baada ya kupata kazi, niliondoka kwa kuhamia pahala pangu peke yangu lakini kila wakati tulikuwa pamoja kwa mashauri na kwa mazungumzo. Baada ya kupata kazi na baada ya kutamakani kidogo, nilileta aila yangu na kuishi pamoja katika maisha yetu mapya.
 
Ole wangu! Kumbe nimeondoka kwa wachinjaji, nimekwenda kwa wala nyama! Baada ya muda wa miezi 16, yaani tangu Juni 1967 mpaka September 1968, tokea kuishi DaresSalaam, nilisitukia ghafla mlango wa nyumba niliyokuwa nikiishi ukigongwa kwa vishindo vikubwa mnamo usiku wa manane, kiasi cha saa saba na nusu hivi. Nilipofungua mlango, waliniingilia ndani watu saba kwa jumla. Watano walikuwa wamevaa nguo za kiaskari wa polisi na walikuwa wame chukua marungu mikononi mwao na wawili, walikuwa wamevaa nguo za kiraia yaani shati na suruali. Wao walikuwa na bastola mikononi mwao. Kiasi cha kuingia ndani tu, waliniuliza, "Jina lako nani?" Niliwajibu, "Aman Thani". Mmoja katika hao wawili waliokuwa wamevaa nguo za kiraia, aliniambia kuwa, "Tokea sasa tumekukamata, na umo katika dhamana ya Polisi". Niliwauliza, "kwa kosa gani?" Nilijibiwa kuwa, "Utaambiwa utapofika Makao Makuu ya Polisi".
 
Niliwaomba waniruhusu kuvaa nguo kwani wakati huo nilikuwa nimevaa shuka na fulana tu. Kwanza walinikatalia na kwa kuwaomba sana, walinikubalia na walimtaka mke wangu aniletee nguo. Niliwahi kuvaa shati na suruali. Nilipokuwa nataka kuvaa soksi na viatu, askari mmoja alinizuwia na alivichukuwa yeye hivyo viatu na aliniambia, "Utavivaa utapokuwa ndani ya gari huko nje".

Niliongozwa na kutolewa nje nikawaacha nyuma mke wangu na mtoto wangu mchanga wa mwaka mmoja katika nchi ya kigeni na katika nyakati za usiku kama huo. Unyonge ulioje! Nilipofika nje, nilizikuta gari mbili za polisi, na nilitiwa katika moja ya hizo.

Yule askari aliyechukuwa viatu vyangu, yeye aliingia katika gari nyengine hakuingia pamoja na mimi. Nilipofika Makao Makuu ya Polisi baada ya kuandikwa jina langu nilisachiwa mwilini na nguoni. Nilipokuwa nikisachiwa nilimwambia huyo aliyekuwa akinisachi kuwa viatu na soksi zangu amechukua mmoja katika askari waliyokuja kunichukuwa kutoka nyumbani kwangu na aliniambia kuwa atanipa wakati nitapokuwepo katika gari nje, lakini sijamuona tena, kwahivyo naomba nipewe viatu vyangu.
 
Jawabu la huyo aliyokuwa akinisachi, lilikuwa, "Hilo mimi halinikhusu, atapokuja, atakuletea". Niliondolewa hapo na nilipelekwa katika vyumba wanavyowekwa mahabusi. Nilipofika huko, niliwakuta baadhi ya Wazanzibari wengine wameshaletwa na ilikuwa kila baada ya muda, wakiletwa wengine mpaka kulipokucha, tulitimia watu 17. Wote isipokuwa mmoja tu, walikuwa ni Wazanzibari.

Huyo mmoja, yeye alikuwa ni mtu wa Tanganyika na hajawahi hata mara moja kwenda Zanzibar wala alikuwa haijui khasa. Wengi ya hao Wazanzibari waliyokamatwa usiku huo, waliondoka Zanzibar na kuishi DaresSalaam miaka mingi nyuma. Wengine zaidi ya miaka 40 walikuwa wakiishi Tanganyika na kufanyakazi huko huko kwa maisha yao yote na hata baadhi yetu hatukuwa tukiingiliana kwa lolote bali hata tulikuwa wengine hatujuani. Usiku kucha tulikuwa macho hapana hata mtu mmoja aliyekuwa angalau amesinzia. Tulikuwa tukiulizana na hapana aliyeweza kumjibu mwenziwe, kwanini tumekamatwa? Tumefanya kosa gani?
 
Kiasi cha saa mbili za asubuhi, alitujia Sajini mmoja pamoja na askari wake na alimwambia huyo askari wake, "Waletee hawa watu chai 'special'". Baada ya muda, tuliletewa chai katika mabirika na vikombe, maziwa, siagi na mikate. Hakika chai ilikuwa chai ya kweli, iliyokuwa imetimia kwa kila kitu. Wakati sisi tukipewa chai kama hiyo, tuliwaona mahabusi wenzetu wengine wakipewa chai kavu na maandazi 43 ya mkahawani!

Tulimuuliza yule askari aliyetuletea hiyo chai, kuwa, mbona sisi tunapewa chai nzuri kama hivi na wale wenzetu wanapewa chai kavu na maandazi na ilhali sisi sote ni mahabusi? Askari alitujibu, "Kweli nyote ni mahabusi lakini nyie ni mahabusi wa kisiasa, na wale ni makriminali. Lazima iwepo tafauti kati yenu".

Kwa kusikia tu neno "wa kisiasa" basi hapo hapo hiyo chai "special" ilitutumbukia nyongo, tuliiona ni "special" kweli! Hapo tena tulianza kutizamana na kila mmoja aliingiliwa na khofu moyoni mwake. Tulikuwa tukiulizana tu wenyewe kwa wenyewe, siasa hizo tumezifanya wapi au za namna gani? Mradi hatukuweza kujijibu kwa lolote.
 
Ilipofika saa sita na nusu mchana, tuliletewa wali wa pilau nzuri na baada ya kumaliza kula, tulichukuliwa mpaka kwenye ofisi moja na huko tulitilishwa vidole (finger prints) na baada ya hapo, tulitiwa katika gari kubwa la polisi na tulipelekwa moja kwa moja mpaka kwenye kiwanja cha ndege za kijeshi. Tulipofika kiwanjani, tulipokelewa na maofisa wawili waliyokuwa hawakuvaa nguo za kiaskari na baada ya kukaa hapo kwa muda mchache, tulitiwa katika ndege ya kijeshi ya aina ya "caribou", tukifuatanishwa na askari watatu wa polisi wote wakiwa wamechukua bastola mikononi mwao. Ndege iliruka na baada ya kiasi cha nusu saa, tuliteremka kiwanja cha ndege cha Zanzibar. Hapo, tulipokewa na askari wa magereza na tulitiwa katika gari la magereza na kupelekwa Makao Makuu ya Magereza, Kiinua Miguu
 
Tulipofika gerezani, tulisachiwa kisha tuliandikwa majina yetu na baada ya hapo, tulikutana na Mkuu wa Magereza, Bwana Adam Taib naye alituambia kama hivi: "Ndugu zangu, mimi nimeambiwa nikopokeeni na nikuwekeni mpaka watapo kuja wenyewe wakubwa. Sijui lolote baada ya hapo. Kwahivyo, msiniulize lolote. Ninalo kuombeni ni kuwa mkae kwa salama mpaka mtapokutana na wenyewe, mtaweza kujua kila jambo". Mpaka tushaletwa Zanzibar, yule askari aliyechukua viatu vyangu na soksi hajafika kuniletea. Ikiwa askari waliopewa dhamana ya kuzuwia ukhalifu usifanyike katika nchi, wao ndio wevi, basi nchi hiyo itakuwa na usalama gani?! Au mwananchi atapata haki yake kutoka wapi?
 
MAHABUSI WADHULUMIWA WA MWALIMU NYERERE
Maalim Harun Ustadh Maalim Mohammed Mattar Seyyid Hassan Sheikh Seyyid Mohammed Adnan Mzee Mohammed Mbaba AhmedRashad Ali Hashim Haji Abdalla Seyyid Hashim Abdalla Baharun AbdulLatif Binbrek Mohammed Shioni Seyyid Mohammed Mattar Mohammed Ali Abbas Ali Abdalla (Admeri) Ali Jaffer Ali Khalifa Miskiry Ali Manara (Mtu wa Tanganyika) Aman Thani Fairooz
 
Baada ya kumaliza kutukhutubia, Mkuu wa Magereza, aliondoka na sisi kila mmoja alipewa kirago chake pamoja na shuka mbili na kopo la kunywiya maji na ndio hilo hilo la kutumia kwa kujisafishia baada ya kwenda haja kubwa na ndogo. Tulipomalizika sote kupewa vitu hivyo, tuliongozwa mpaka kwenye vyumba vya kulala mahabusi. Siku ya pili, waliletwa wenzetu wawili wengine, mmoja alikuwa mwanamke, Bibi Mbarawa Bakari, yeye alipelekwa katika upande wa mahabusi wa kike na mwengine alikuwa Seyyid Harun Abdalla Baharun, yeye aliletwa upande wetu. Sote kwa jumla tukawa watu 19, mmoja mwanamke na 18 wanaume. Hawa wenzetu wawili, Bibi Mbarawa na Seyyid Harun wao walikamatwa hapo hapo Zanzibar
 
Mpaka wakati 44 huo tulikuwa bado hatujaweza kufahamu sababu zilizopelekea kukamatwa na kuletwa gerezani. Baada ya kiasi cha mwezi mmoja tokea kuletwa gerezani, Rais Karume pamoja na kikosi chake cha 'Baraza la Mavamizi' walikuja na Karume alitukhutubia kwa kutumia maneno kama haya:

"Nyinyi mmeletwa kwetu kutokana na ukorofi mnaoufanya huko DaresSalaam. Mwalimu Nyerere ametoa amri muondolewe na mrejeshwe makwenu. Mpaka sasa bado hatujaletewa ripoti yenu kamili. Tutapoipata na baada ya kuichunguza, tutatoa uamuzi wetu. Ikiwa kukuachilieni huru au kukupelekeni mbele ya mahakama. Lakini mjue kuwa mahakama yenyewe ni ya kijeshi. Ikiwa mutaonekana na kosa, basi adabu yenu itakuwa KIFO".
 
Baada ya kusema hivyo, alianza kututukana na kututisha kwa kutumia lugha za ukali na za vitisho na alielekeza matusi yake na vitisho vyake zaidi kwa ndugu zetu wenye asili za Kingazija kwa vile ilitokea katika hilo kundi letu, jamaa wa Kingazija walikuwa wakionekana ni wengi. Kutokana na vitisho hivyo, ndugu yetu mmoja aliingiwa na khofu hata alitokwa na haja ndogo bila ya kuweza kujizuwia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…