D A E M U S H I N
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 22,665
- 121,102
KIASI CHA KAZI ALICHOKUWA AKIFANYISHWA MFUNGWA
Ikiwa kazi ni ya kupiga matuta ya muhogo, kila mfungwa alikuwa akitakiwa kupiga tuta moja unusu kwa siku, (tuta moja unusu inakuwa, tuta zima la mfungwa peke yake na tuta la pili la kushirikiana wafungwa wawili). Ukubwa wa tuta hilo ilikuwa ni kiasi cha yadi 150 urefu, yadi moja upana na kunyanyuka kwenda juu kiasi ya yadi moja. Ikiwa kazi ni ya kulima katika konde ya mpunga,
kila mfungwa hupewa ngwe yake. Urefu wa ngwe ni kiasi cha yadi 150 mpaka 200 na upana kiasi cha yadi tatu. Ikiwa kazi ni za kun'goa minazi, kila mfungwa akitakiwa kwa siku ang'owe na kuipanguwa (kuikata mapande mapande) minazi miwili mpaka mitatu. Ikiwa kazi ni kuchimba mawe, kila wafungwa watatu wakitakiwa wachimbe mawe na waijaze mita yao. (mita hiyo ilikuwa na kipimo chenye urefu wa kiasi cha futi nane, upana wa futi nne na kunyanyuka kwendea juu kiasi cha futi tano.