Shimba ya Buyenze
JF-Expert Member
- Dec 22, 2014
- 183,580
- 1,105,911
Kama ni mke wake...na kama huyo mke ana akili na anajitambua sioni tatizo. Tena watafanikiwa sana na ndoa yao itadumu...Nipeni mbinu nijinasue, mke wangu ananiendesha kama gari bovu
Jamani nisaidie, Nikitoka kazini najikuta nakabidhi tu hela kirahisirahisi kwa mke wakati awali haikuwa hivyo. Simu yangu alikuwa hagusi lakini sasa hivi imekuwa kama yake Ananipelekesha si mchezowww.jamiiforums.com
Baharia ameshikika [emoji23][emoji23]
Wanaume wengi hawana mazoea hayo, ya kuwa open kwa wake zao...na ikitokea unaona wanavyohaha kama huyo.!Kama ni mke wake...na kama huyo mke ana akili na anajitambua sioni tatizo. Tena watafanikiwa sana na ndoa yao itadumu...
Ila kama ni mchepuko basi baharia kwishnei
Tena hii inabidi iwe applied hii december[emoji23][emoji23][emoji23]
Kuna watu wanajua kujikausha bhana[emoji16][emoji16]Unakuta na malapa nje kabisa
Amen[emoji2088][emoji2088][emoji2088][emoji2088][emoji2088]Don't end this year holding secrets, tell your girlfriend you won't marry her [emoji57]
AiseeKUREJESHEWA UHURU WETU
Taarikhi 9 Januari, 1972 katika nyakati za asubuhi, Karume pamoja na kikosi chake cha Baraza la Mavamizi walikwenda kwanza katika Makao Makuu ya Magereza, Kiinua Miguu na baada ya kuwakhutubia wafungwa huko walikuja shamba katika gereza la Langoni. Walipofika hapa Karume alitukhutubia kwa kutuambia,
"Leo tumekuja kukuachilieni huru wafungwa wote na tumeamua kuyafunga magereza yote na badala yake, tutafungua Vyuo vya Mafunzo katika sehemu hizi hizi za magereza. Ingawa tokea hii leo nyote ni huru lakini mtabakia humu humu magerezani mpaka siku ya taarikhi 12 Januari, siku ya kusherehekea Mapinduzi, ndio siku mtaoachiliwa kwenda majumbani mwenu".
Baada ya kumaliza kusema maneno hayo, Karume kama kawaida yake alianza kutoa porojo lake lisilo miguu wala kichwa, alipochoka mwenyewe alinyamaza, na aliondoka pamoja na kundi lake na kutuacha sisi katika hali ya furaha na kumshukuru Mwenyezi Mungu.
Aisee...Miongoni mwa waliokamatwa wakati huo walikuwa Mabwana hawa: (akiwemo bibi mmoja) Muhammed Salim (Jinja) Amour Zahor Said Dahoma (Kombanyongo) Mohammed Hamoud Barwani Nasser Mansour Musa Ahmed (Lashoka) Sultan Binbrek Ali Mohammed Barwani Bibi wa Unguja (Mke wa Bwana AbdulRahman Haider[ Maalesh]) Mohammed Salim Jinja, Amour Zahor, Said Kombanyongo, Mohammed Hamoud na Hamza Mohammed, wao ndiwo walioondolewa kutoka Makao Makuu ya Magereza na kupelekwa "Army House". Tokea siku hiyo waliyoondoshwa kutoka Makao Makuu ya Magereza hadi hii leo hawa jaonekana tena. Kutokana na khabari zenye kuaminika na hao wenziwao waliyokuwa pamoja wakati huo zinasema kuwa wote hao 53 yaani Mohammmed Salim Jinja, Amour Zahor, Said Kombanyongo, Mohammed Hamoud na Hamza Mohammed, wameuliwa siku moja katika sehemu ya Kama, Unguja kwa kupigwa risasi.
Duh!! ........(2) Maalim Harun Ustadh
Wakati tulipofungwa gerezani, Maalim Harun alikuwa akikurubia miaka 70 na siha yake tokea kabla ya kufungwa haikuwa nzuri kutokana na umri wake na maradhi aliyokuwa nayo, presha na ugonjwa wa miguu. Lakini kwa kuwa alikuwa akipata matibabu yaliyokuwa bora na vyakula vyenye kutengeza viwiliwili vya binadamu, na alikuwa na uhuru wake ekenda huku na huku aliweza kuishi kwa uzuri.
Kwa kufungwa na kuyakosa yote hayo, na juu yake kufanyishwa kazi zisizokuwa kadiri yake kutokana na umri wake na maradhi aliyokuwa nayo, kila siku uchao alikuwa akizidi kudhoofika. Mambo yalipomzidia, alianza kukohoa na kutoka damu katika makohoo.
Baadae alianza kuvimba miguu na uso na kupata shida ya kuvuta pumzi. Bwana Mganga wa gereza la Langoni, alitoa pendekezo la kutaka apelekwe Maalim Harun hospitali kuu kwa kukutana na Daktari mkuu, Muhidini Khamis Kwangwati mkuu wa gereza hilo la Langoni na Kinu Moshi kama kawaida yake alipinga na alimuacha Maalim Harun hapo hapo gerezani akiatilika na maradhi
. Alipofika hali ya kuchungulia kaburi kwani alikuwa hata akisema, maneno hayatambulikani sawa sawa na kutoweza hata kujisaidia mwenyewe, ndipo hapo alipoondolewa na kupelekwa katika hicho kihospitali cha Makao Makuu ya Magereza, Kiinua Miguu. Na huko haukuchukua muda ila naye aliiaga dunia kama alivyoiyaga mwenziwe Mzee Mbaba.
Duh!............(3) Idi Hassan
Huyu ni kijana wa kiMakunduchi, aliwahi kuwa Inspekta wa polisi. Alipostaafu alijiunga na AfroShirazi na alikuwa miongoni mwa wakereketwa wakubwa wa AfroShirazi. Baina ya 1970 na 1971, Idi aliletwa gerezani, Langoni kwa kifungo cha miaka 10 baada ya kuwekwa katika gereza la "Kwa Ba Mkwe" kwa muda mkubwa. Alipoletwa gerezani alikuwa katika hali mbaya ya siha yake kwani kwa mujibu wa kauli yake mwenyewe alisema kuwa Mandera alimtesa sana kwa kumpiga na kwa mengineo. Idi baada ya muda mdogo tokea kufungwa, alipata maradhi ya kifua kikuu (TB). Siku moja ghafla alipokuwa anarejeshwa kutoka kufanyishwa kazi, alikohoa na kutapika mapande, mapande ya damu. Kiasi cha kwenda kuitwa Bwana Mganga kutoka kwenye 'dispensari' ya Kizimbani, alipofika alimkuta Idi zamani ameshaondoka duniani.