Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hii ni ban karibia ya 3 katika hizi wiki mbili. Sijui ni ligi za kule celebrity forum. Sijui ni nini sasa. Akiwapo hapa huwa kunachangamka sana. Hata Kazaramo huwa kanajitokeza mara kwa mara [emoji16][emoji16][emoji16]
Ni kweli bro,huwa wanachangamsha sana hasa wakianza zile story zao ubuyu na pages mbalimbali za insta..uzi huwa unakuwa on fire..

Sijui nini shida ila kuna mahali nilimuona kwenye uzi flan hv siukumbuk,ulikuwa uzi wa kuwaponda mods kuwa hawatak kuambiwa ukweli,pia wanafuta futa comment pasipo kuwa na sababu yoyote ile..nahisi huu uzi ndio chanzo cha hii ban,maana mleta uzi mwenyew alikuwa amejilipua kwa lolote [emoji16][emoji16]
 
Ni kweli bro,huwa wanachangamsha sana hasa wakianza zile story zao ubuyu na pages mbalimbali za insta..uzi huwa unakuwa on fire..

Sijui nini shida ila kuna mahali nilimuona kwenye uzi flan hv siukumbuk,ulikuwa uzi wa kuwaponda mods kuwa hawatak kuambiwa ukweli,pia wanafuta futa comment pasipo kuwa na sababu yoyote ile..nahisi huu uzi ndio chanzo cha hii ban,maana mleta uzi mwenyew alikuwa amejilipua kwa lolote [emoji16][emoji16]
Aisee. Hata mabaharia wa Kula Tunda kwa Masikhara kule nao wanatukana balaa kuwa meseji zao zinafutwa. Ni malalamiko tu mtindo mmoja...

Basi kutakuwa na mod mkorofi ameamua kula sahani moja na Binti Mpole...
 
Wachina shwaini zao....
447824301_175916.jpeg
 
KARUME KUANZA KUMBADILIKIA TWALA
Katika kuendelea na mazungumzo yetu baina yangu na Abdul Aziz Twala, aliniambia kuwa mwanzoni yeye alikuwa katika hao watoto wazuri mbele ya Mzee Karume, na ilikuwa kila alichokuwa akikitaka kwa Karume akikipata bila ya taabu yoyote. Mambo yalianza kuharibika wakati ujumbe wa Serikali ya Mavamizi ulipoalikwa Misri.
 
Twala amesema kuwa alipokuwa akitengeneza kutoa matumizi ya safari (travelling allowances) kwa wajumbe wa safari hiyo, aliwacha kumtia katika orodha ya matumizi ya safari Bibi Fatma Karume kwa sababu Bibi Fatma alikuwa anachukuliwa na mumewe kwa matembezi tu, sio katika ujumbe rasmi. Mzee Karume, alipoona mkewe hakutengenezewa sehemu yake ya matumizi, alimuuliza Waziri wake wa Nchi kukhusu posho la mama Fatma Karume.
 
Twala alipigiwa simu na Waziri wa Nchi, AlHaj Aboud Jumbe na alimwambia,
"Mbona umesahau kuleta posho la mama Fatma Karume?"
Twala alimjibu, "Laa, sikusahau lakini nimeona kuwa yeye si katika wajumbe rasmi wa safari. Lakini, ikiwa unaona na yeye anastahiki, basi nitamtengenezea".

Twala amesema haukupita muda baada ya mazungumzo hayo ila alipata simu nyengine kutoka kwa Katibu wa Waziri wa Nchi kumwambia kuwa, "Unaambiwa na Mzee basi usilete posho la mama Fatma. Yeye mwenyewe atampa kutoka mfukoni mwake".

Twala amesema kutokana na jawabu hilo la Mzee, alihisi kuwa amesha mtonesha Mzee kidonda; na kweli ndivyo ilivyokuwa. Kutoka wakati huo mambo yalianza kuharibika, alisema Twala. Ujumbe uliporejea Misri, Twala amesema kuwa kila alipokuwa akikutana na Mzee Karume alikuwa hampi mkabala mwema.
 
Jambo jengine ameniambia Twala lililozidi kutimua mavumbi lilitokea wakati mmoja alipokuwa Mwalimu Nyerere amehudhuria kikao cha Baraza la Mavamizi (baraza la mapinduzi). Katika kikao hicho, amesema Twala, Mwalimu alilaumu kukhusu namna zilivyotumiwa fedha za kigeni kwa kununulia vitu kwa wingi kama peremendi, tofi, chakileti, ubani wa kutafuna na vyenginevyo ambavyo havikuwa na umuhimu katika maisha ya binaadamu wakati yapo mambo mengi muhimu yanayohitajia fedha za kigeni.
 
Twala amesema kuwa Karume alivyomuona Mwalimu akilaumu kiasi hicho, alinigeukia na aliniambia, "Mheshimiwa Waziri wa Fedha, unasikia maneno hayo? Usijitumilie mapesa ovyo ovyo tu".

Twala amesema, siku hiyo alishindwa kunyamaza kimya, alisema kujibu hayo, "Kweli mimi ndiye niliyempa amri Waziri wa Biashara na Viwanda, Sheikh Shaaban Soud Mponda aagizie vitu hivyo, lakini nimefanya hivyo, baada ya kupata amri kutoka katika ofisi yako ya kunitaka mimi nitowe idadi fulani ya fedha kwa kuagizia vitu hivyo kutoka Ujarumani ya Mashariki. Sasa mimi Mzee, kosa langu ni lipi hapo?
 
Twala ameniambia kuwa, alivyokuwa amesema hivyo, alimuona Karume amesawijika uso, na alikuwa akipuma kama n'gombe jike. Mwalimu alipoona hali haikuwa nzuri, alijaribu kuyageuza mazungumzo na kuleta maudhui nyengine. Mkutano ulipomalizika, Mwalimu aliondoka kurejea DaresSalaam. Siku ya pili yake, amesema Twala, kiasi cha kuingia katika ofisi yake, alipata simu kutoka kwa Waziri wa Nchi ya kumwambia kuwa kutakuwepo na mkutano wa dharura katika Peoples' Palace na wote wahudhurie.
 
Twala amesema kwa kupata khabari kama hizo tu basi nusra alikuwa atokwe na mkojo suruwalini! Alipofika kwenye mkutano, Twala amesema aliwaona baadhi ya wenzake hawakuwa na mtizamo mzuri juu yake. Kila mmoja alikuwa akimuepuka epuka.

Alipoingia Mzee Karume na kwa namna alivyomuona, alisema Twala, aliona kuwa leo patakuwa na kazi hapa. Karume aliufungua mkutano kwa kusema, "Nimekwiteni kwa ghafla ili tupate kuyazungumza pamoja na kuyazingatia mazungumzo ya jana aliyoyazungumza Mwalimu Nyerere hapa, na namna mlivyomsikia Mheshimiwa Twala alivyoweza kunivua nguo na kuniacha uchi mbele ya mzee mwenzangu.

Ninakuapieni kuwa jana sikuweza kupata usingizi, usiku kucha nimekaa macho nikifikiri vipi Mwalimu ataniona. Kwani mimi nilikuwa sijui kuwa amri ya kuagizia vitu hivyo nimeitoa mimi? Najuwa, lakini, ilivyokuwa maneno aliyosema Mwalimu yalikuwa na uzito, niliona bora kosa hili nimtupie mwanangu ili mimi mzee nipate kusitirika, lakini sikujuwa kuwa mwanangu ndiye ataye nifedhehesha zaidi"
.
 
Twala ameniambia kuwa hapo Karume alianza kuwatolea hadithi za watoto wa kizamani walivyokuwa na adabu mbele ya wazee wao. Karume alisema kuwa, "Wakati mwengine hutokea mzee katika baraza akatokwa na pumzi, kujamba mbele ya wazee wenziwe na ilikuwa likitokea jambo kama hilo, akitupiwa mtoto yoyote aliye kuwepo hapo, na mtoto akiwa hata yeye siye aliyefanya hivyo alikuwa hakatai, wala alikuwa hasemi chochote. Akinyamaza kimya! Baraza inapo malizika na wazee wakatawanyika, yule 61 mtoto alikuwa akipewa pesa moja au mbili akanunue kashata au chochote akipendacho kwa kuwa amewasitiri wazee wake. Na hivyo, ndivyo nilivyo tumainia kuwa mwanangu ataweza kunisitiri, lakini kanifedhehisha zaidi. Bora ningelinyamaza kimya kuliko vile nilivyokuwa nimesema".
 
Alipokuwa akiendelea kusema hayo, Twala ameniambia, aliwaona wenzake wakitikisa tikisa vichwa kwa kuonesha wana masikitiko makubwa juu ya hayo yaliyofanyika. Baada ya Karume kumaliza kusema aliyotaka kuyasema, aliliuliza Baraza lake, "Sasa kijana kama huyu afanywe kitu gani?" Twala ameniambia kuwa, hakukutokea hata mwenzake mmoja aliyesema maneno ya kuonesha kumtakia rehema. Kila aliyekuwa anasema, akizidi kumshindilia ili Karume azidi kumuona ni mtu mbaya. Baada ya muda, Twala amesema, Mzee Karume alisema, "Leo, nakusamehe Twala. Adabu ninayokupa ni ya kukuondoa kwenye Wizara ya Fedha, kuanzia leo, kesho nakutaka ukakamate Wizara ya Afya. Kuanzia leo Wizara hii ya Fedha itakuwa chini yangu".
 
Back
Top Bottom