Hapana wasia kwa warithi (muhammad bin abdillah)
kwa sheria za kiislamu
Sheria ya Islam imeweka sehemu maalumu kwa ajili ya jamaa fulani ya karibu katika mali yanayoachwa na maiti. Mathalan, mke katika hali moja anapokea sehemu ya nne (1/4) ya urithi wa mumewe marehemu na katika hali nyingine apata sehemu ya nane (1/8).
Hiyo ni amri ya Mwenyezi Mungu na mumewe hana haki ya kumwongezea kitu cho chote. Naam, anaweza kufanya wasia wa thuluthi ya mali yake kumpa rafiki zake au jamaa zake wasio na sehemu maalumu katika urithi au mayatima au kwa ajili ya dini. Kwa njia hii M wenyezi Mungu amezuia mtu ye yote asipokee mali nyingi peke yake. Watu wengi wakipata mali kidogo ni bora zaidi kuliko mtu mmoja kupata mali yote. Ndiyo njia ya amani, raha, na starehe.