moudgulf
JF-Expert Member
- Jan 23, 2017
- 159,165
- 777,891
Hapana wasia kwa warithi (muhammad bin abdillah)
kwa sheria za kiislamu
Sheria ya Islam imeweka sehemu maalumu kwa ajili ya jamaa fulani ya karibu katika mali yanayoachwa na maiti. Mathalan, mke katika hali moja anapokea sehemu ya nne (1/4) ya urithi wa mumewe marehemu na katika hali nyingine apata sehemu ya nane (1/8).
Hiyo ni amri ya Mwenyezi Mungu na mumewe hana haki ya kumwongezea kitu cho chote. Naam, anaweza kufanya wasia wa thuluthi ya mali yake kumpa rafiki zake au jamaa zake wasio na sehemu maalumu katika urithi au mayatima au kwa ajili ya dini. Kwa njia hii M wenyezi Mungu amezuia mtu ye yote asipokee mali nyingi peke yake. Watu wengi wakipata mali kidogo ni bora zaidi kuliko mtu mmoja kupata mali yote. Ndiyo njia ya amani, raha, na starehe.
Subira ni ridhaa (muhammad bin abdillah)
Subira siyo kuvumilia taabu na hali mna mnungβuniko moyoni. Bali hakika ya subira, kama alivyosema Mtume, ni kuridhika na tendo la Mwenyezi Mungu liwe la kutupendeza au kutuchukiza.
Dunia ndivo konde la Akhera (muhammad bin abdillah)
Kila mtu ni mlimaji na cho chote atakachotenda katika maisha ya dunia mfano wake ni kama mbegu ipandwayo kondeni na yeye atakwenda kuvuna matunda yake baada ya kufa kwake. Basi na aangalie apandacho.
Na livapuliiii?Atletico Madrid siyo timu ya kubeza,
Ni timu yenye uwezo wa kugeuza mambo ndani ya uwanja,
Ni timu inayopaswa kuheshimiwaView attachment 1294740View attachment 1294741
Sent using Jamii Forums mobile app
Kupeleka rambirambi kuwe mara moja tu (muhammd bin abdillah)
Ni desturi mbaya kukusanyika mahali pa matanga na kukaa hapo hapo siku nyingi kuwatia gharama waliofiwa. Mtu aliyepatwa na msiba lazima apewe mkono wa tanzia maana atafarijika lakini kuiendeleza muda mrefu kutamwongezea huzuni na mzigo.
Jifunzeni yakin (muhammd bin abdillah)
Yakini maana yake ni kujua jambo fulani kwa hakika kuwa ndivyo. Yakini ndiyo msingi wa matendo yote. Mtu mwenye yakini kuwa mbegu zikipandikizwa zitaota ndiye anayeweza kuzitoa ghalani na kuzifukia ardhini. Watu ambao imani yao inalewalewa hawafiki mahali.
Kuaminiwa ni heshima (muhammd bin abdillah)
Yafaa Mwanadamu akae duniani kwa jinsi itakayompelekea kuaminika. Mtume s.a.w. alipewa lakabu ya βAlaminβ (mwaminifu) na watu wake tangu alipokuwa kijana kwa sababu ya maisha yake yaliyotukuka. Mhaini hana heshima.
Waheshimuni watoto wenu (muhammd bin abdillah)
Mtoto wa leo ni baba wa kesho. Lazima tuwafunze kujiheshimu na hivyo watakuwa na moyo wa kujitoa katika yale yanayowaletea aibu na pia watashika adabu njema ya kuwaheshimu wengine, wakubwa kwa wadogo. Kuwatolea ukali kila mara si vizuri.
Nawausieni juu ya jirani (muhammd bin abdillah)
Dini ya Kiislamu imetia mkazo juu ya kuwatendea wema majirani. Jirani na awe mtu namna gani anastahiki kuangaliwa vizuri. Kuoneana huruma hukuza mapenzi na amani.
Linda ulimi wako (muhammd bin abdillah)
Yaani usiwe na masingizio, uongo, utesi na maneno ya magomvi, machafuko, na maneno ya upuuzi
Duh!! walitegemea zawadiRIP Mr and Mrs. Odipo [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
View attachment 1294758
Ogopeni masikhara, kwa sababu yanapunguza uungwana na uanaume.
π π πTumshukuru Mwenyezi Mungu kwa baraka zake kutujaalia kuamka salama
Sent using Jamii Forums mobile app
π πβMsicheke sana kwa sababu kucheka sana kunaua moyo wa mtu.