Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mbwa mwitu ni wanyama wawindaji wanaokula nyama, ni wanyama wafupi na wadogo kimuonekano, huishi katika makundi makumbwa sana, urefu wa kutoka miguuni hadi begani huweza kufikia inches 35 tuu na hiyo ni kwa wale ambao wakubwa, lakini urefu wa kichwani mpaka mkiani hufikia inches 55, kwa vipimo hivi unaweza kuona wanyama hawa ni wadogo kiasi gani kwa maumbo yao, lakini kama vipimo hivyo ni mtihani basi kukurahisishia nakwambia hivi, mbwa mwitu kwa umbo ni mdogo zaidi kwa mbwa tunaowafuga.
 
Wanyama hawa huishi katika vichaka na sehemu majani makavu makavu, hubeba mimba kwa miezi mitatu na siku chache kidogo kama atazidisha, na hawana idadi maalumu ya watoto anaozaa hapa hutegemea dume lilikuwa na mbavu kiasi gani, lakini kwa kifupi huzaa watoto wengi, watoto hukaa chini ya uangalizi wa mama kwa kwa miezi mitatu na baada ya hapo huanza kujitegemea, wanapofikisha mwaka mmoja majike huanza kunusa harufu ya kuitwa mama, maana huanza kuyadondosha mate madume, kwa muonekano wao mzuri na wakuvutia.
 
Tabia yao ya umoja, kushirikiana huwafanya waonekane ni wababe wa mji, wanyama hawa huogopwa hata na wanyama wenzao wanao winda kwani bifu lao huwa ni lakufunga mtaa, hata simba akiwaona mkia wake huuficha, usiseme kwa fisi nk, huweza kukimbia umbali wa km 71 kwa saa, hivyo kaa ukijua ni viumbe ambao wana hatari sana wakati mwingine humla mnyama wakati wanamkimbiza.
 
wakati mbwa wa kiAfrika wanapokwenda kuwinda wakiongozana pamoja na kufukuza pamoja windo lao, wolf hugawana njia na mmoja wao anapoona windo huanza kwa kulizubaisha akilikenulia meno na kutoa sauti ambayo wenzao hutambua kuwa wanaitiwa nini,
 
Mbwa mwitu ni wanyama wanaokula nyama na wanyama wanaopendelea kuwawinda ni pamoja na paa, mbawala, nyumbu,pundamilia nk pamoja na wanyama hao lakini pia huweza kuwawinda wanyama wakubwa ambao hata simba huwaogopa kama nyati na twiga nk.
 
Back
Top Bottom