MEEK MILL AJIONDOA INSTAGRAM KWA MUDA KISA MJADALA HUU | _ Moja ya Habari inayotrend kwa sasa unyamwezini ni tetesi za rapa Meek Mill kudaiwa kupata mtoto na anayedaiwa kuwa mpenzi wake Milano japo wawili hao wamekuwa wakikana kuwa sio wapenzi zaidi ni urafiki tu. Kitendo hicho cha watu kuendelea kumsumbua kutaka kujua kama ni kweli wawili hao wamepata mtoto kimemfanya hadi Meek Mill kuondoa akaunti yake ya instagram kwa muda na kuhamia Twitter ambako huko ameandika ujumbe unaosemeka kuwa "Kweli ni Mtoto wangu" Hebu niambie ni jambo gani linaloweza kupelekea wewe kujitoa kwenye instagram yako? -
Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta ana matumaini kuwa Granit Xhaka, 27, hataondoka klabu hiyo mwezi Januari licha ya kiungo huyo wa Uswizi kuhusushwa na tetesi za kujiunga na Hertha Berlin ya Ujerumani. (Football.London)
Manchester United ilimpatia ofa kubwa zaidi Erling Braut Haaland lakini mshambuliaji huyo wa Norway wa miaka 19, aliamua kujiunga na Borussia Dortmund ili aendelee kukuza kipaji chake(Independent)
Mkufunzi wa Chelsea, Frank Lampard amesema klabu hiyo inashauriana na Tariq Lamptey, 19, anayecheza safu ya kulia na nyuma kuhusu mkataba mpya huku mkataba wake wa sasa ukitarajiwa kukamilika mwisho wa msimu huu. (Goal)
Arsenal lazima itangaze ofa ya kisawasawa kuishawishi Atletico Madrid kumuuza kiungo wa kati wa Ufaransa Thomas Lemar, 24, mwezi Januari. (AS, via Mirror)
Arsenal na Tottenham zinajiandaa kulipa £50m kumsajili beki wa kati na nyuma wa RB Leipzig, mfaransa Dayot Upamecano, 21, lakini huenda wakakabiliwa na ushindani kutoka kwa Manchester City. (Daily Star)
Newcastle inashughulikia mpango wa kurefusha mkataba wa kiungo wake wa kati Jonjo Shelvey, 27, ambaye mkataba wake wa sasa unaendelea hadi mwaka 2021. (Chronicle)
Fiorentina huenda ikasitisha mapema mkataba wa mkopo wa winga wa Leicester na Algeria Rachid Ghezzal,27, ambao ulikuwa uendelee kwa msimu mzima huku klabu ya Atalanta ya Italia ikitarajiwa kufaidi kutokana na hatua hiyo. (La Gazzetta dello Sport, via Leicester Mercury)
Mkufunzi wa Everton Carlo Ancelotti amesema amekuwa akimfuatilia mshambuliaji wa Toffees Dominic Calvert-Lewin akiwa katika vilabu vingine lakini hakuwahi kupata nafasi ya kumsajili mchezaji huyo wa miaka 22. (Liverpool Echo)
Atletico Madrid huenda ikamsajili mshambuliaji wa Beijing Guoan, Cedric Bakambu, 28, mwezi Januari ikiwa watashindwa kusaini chaguo lao la kwanza Edinson Cavani, 32, kutoka Paris St-Germain. (Mundo Deportivo - Kwa Kihispania)
Mkufunzi wa Newcastle Steve Bruce amesema hatawasajili wachezaji wapya mwezi Januari kwa lengo la kushughulikia changamoto ya majeruhi inayowakabili wachezaji wake . (Mail)
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.