Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Heri na baraka za Muumba ziwe nasi kwenye mwaka huu wa Ishirini Ishirini[emoji120][emoji120]
FB_IMG_1577862994699.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanafamilia;

Tayari tumo 2020. Wuhuuu [emoji1734][emoji1734][emoji1734][emoji1734]

View attachment 1308946

Mungu Ametujalia sana na kutupa upendeleo wa ajabu. Tumeuona mwaka mpya (2020). Hebu basi mwaka huu na ukawe wa mibaraka, amani, upendo na utangamano zaidi.

Kwenu bros wote (hasa The King, Kijana Mpole, Ninge, Bradha, Mkokaa na Mfilisti) - love you guys. Bila nyinyi uzi huu utakosa ladha kabisa. Kwa wanaharakati wetu katika uzi huu (hasa Coco na BAK) - endeleeni kupambana mpaka kieleweke na 2020 ndiyo hii.

Kwa Sis wangu wa pekee hapa - dumisha upole na amani yako. Wewe u mfano wa kuigwa. Jirani Yetu Mwema. Endelea kutuombea kwa Molla wetu na kutupa pole bila kuchoka. Wewe ndiye mleta farijiko letu hapa.

Esta. Kusema kweli wewe ndiye injini ya uzi huu. Natumaini 2020 tutaendelea kuwa nawe hapa; na ban zisizo za lazima zitakuepuka. Shemeji yangu kipenzi (aka TRM Kivuruge). Ukiwepo hapa uzi huu huwa unachangamka sana. Najua una majukumu mengi lakini kama anavyosemaga King himuselfu - muda ukipatikana basi tunakutana hapa. Mtazamo wako chanya na posti zako nyingi za kutia moyo huwa zinatubariki wengi. TH mcheshi usiye na makuu. Endelea kuwa nasi. Andaeitini wa Arachuga - busara zako za kiandaeitini na fikra zako komavu pamoja na mitazamo yako chanya bado inahitajika sana katika uzi huu.

Mpendwa wetu Hawachi. Wewe ni mpendwa wa uzi huu na ni mmoja wa watu wanaoheshimiwa sana hapa JF. Japo ulikuwa mkimya ila mwishoni hapa umeweza kufunguka na kuanza kutaniana na kila mmoja japo kwa viwango. Endelea hivyo kwa mwaka huu ili upendwa wako ukaweze kudhihirika zaidi na kutubariki.

Poti unatuhumiwa kuwa umebadilika. Sijui huko ulikokuwa watekaji wamekufanya nini. 2020 tunamtaka poti wetu tuliyemzoea. Poti mbeba maua, magauni ya bluu, viatu vya mchuchumio na makreti ya mvinyo. Tunaomba ucheshi wako urudi. Mishil - moyo wako wa kutokata tamaa na ukaendelee na 2020 hii ikalete utimilifu katika harakati zako zote.

Kwa Wahenga Wenzangu - busara zenu bado zinahitajika sana na mkiona kitu hakijaenda sawa, msikose kutoa mtazamo wenu. Ankoo una uwezo mkubwa wa kiushawishi na zaidi ya mara moja uliwahi kunichomoa kutoka kwenye iginoa listi. Wewe pia ni mwanafalsafa mbobevu na japo huwa unaaandika kidhihaka dhihaka na kiucheshi sana, jumbe zako nyingi huwa zimebeba busara na hekima nyingi ndanimwe. Tunakutegemea sana katika uzi huu kwa mambo mengi.

Kwenu Mashabiki wa Livapuu. Ni wazi mwaka huu ni wenu. Japo ushabiki wenu unakera sana, nawaombea moto wenu usizimike na mwaka huu muweze kutimiza ndoto zenu za muda mrefu na hatimaye muweze kulitwaa kombe la EPL.

Kwenu mliopotea katika uzi huu (na wengine ambao sikuwataja) - Fragaria, Prof, Ledada, Jakitoo, BAK na wengineo, Mungu Awabariki sana huko mliko. Na muda ukipatikana basi msikose kupita hapa kutusalimia.

Binafsi sina kinyongo na mtu hapa na kama kuna mtu ambaye kwa namna moja au nyingine nilimkosea basi naomba msamaha wa dhati. Tuanze mwaka mpya katika upya wake, na kama ambavyo jirani yetu huwa anatukumbusha kila mara, amani na upendo wetu vikadumu. Kwa sasa niko napambana na kijukumu fulani hivi lakini kwa msaada wa Mungu naona karibu kitakamilika; na mambo yakikaa sawa kabisa kwa asilimia mia basi nitarudi tena hapa kwenye uzi wetu kwa ari mpya na nguvu mpya

Blessings and Happy New Year Wanafamilia.

View attachment 1308947
Happy New year The don.....Asante kwa moyo wako wa upendo pamoja ujumbe mzuri kwetu[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Karibuni kwangu ni kule kayenze juu,panda gari za igombe pita kilimahewa,iloganzala,sabasaba etc pandisha mibuyuni misunguni bapayonaza ukisikia harufu ya pilau basi ni hapo hapo karibuni sana.

NB kila mtu aje na mboga yake
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom