Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Buns za nyama ndani MAHITAJI: Chumvi vijiko viwili vya chai Sukari vijiko viwili vya chai Amira ya chenga vijiko viwili vya chai Siagi iliyoteyushwa vijiko vinne vya chai Unga wa ngano vikombe vinne Maziwa ya maji ya vuguvugu kikombe kimoja Mayai mawili MAHITAJI YA NYAMA: Nyama ya kusaga yoyote nusu kilo Mafuta ya kupikia vijiko viwili vya chai Tangawizi na kitunguu saumu kilichopondwa kijiko kimoja Soy sauce kijiko kimoja kikubwa ( optional) Maji ya limao au ndimu kijiko kimoja cha chai Nyanya ya pakti vijiko viwili vikubwa Mtindi vijiko viwili vya chai Pilipili manga ya unga nusu kijiko cha chai Chumvi Ufuta vijiko vitatu vikubwa ( kama utapenda) Yai moja JINSI YA KUPIKA: 1) Katika bakuli pana weka maziwa, chumvi, sukari, amira koroga vichanganyike na uache kwa dk 10 kisha mimina siagi na vunjia mayai na tumia mchapio au hand mixer kuchanganya mpaka vichanganyike 2) Halafu anza kuweka unga weka kikombe kimoja kimoja huku unaendelea kuchanganya upate donge kanda lilainike kisha funika kwa saa moja liumuke 3) Chukuwa nyama yako ya kusaga weka katika bakuli kisha weka soy sauce, maji ya limao au ndimu, chumvi, mtindi, pilipili manga , tangawizi na kitunguu saumu kisha changanya na uifunike kwa nusu saa 4) Baada ya nusu saa weka pan jikoni weka mafuta yakipata moto kiasi mimina nyama yote na anza kuigeuza geuza ikianza kukauka maji weka nyanya na endelea kuipika mpaka iwe kavu iive kisha epua 5) Chukuwa unga wako ulioukanda ukaumuka anza kukata madonge, kisha chukuwa donge moja tumia vidole kulisukuma upata nafasi ya kuweka nyama kisha weka nyama ya kutosha na ufunge donge lako vizuri kama tunavyofanya katika chapati za kusukuma fanya hivyo madonge yote yaishe kisha yapange katika trey la oven acha nafasi kati ya donge moja na lingine ili yapate nafasi wakati wa kuoka yafunike tena kwa nusu saa 6) Baada ya nusu saa Chukuwa yai moja weka katika bakuli na maji kidogo lipige kisha Pakaa juu ya madonge yako na unyunyizie ufuta juu ya madonge yote 7) pre heat oven kwa dk 30 katika moto wa 200C halafu uoke -
 
KASHATA ZA MAZIWA(FUDGE) Siagi 1/2 kikombe / blueband Sukari kikombe 1 Maziwa mazito (condensed milk) kikopo 1 kama huna si lazima Maziwa ya maji 1/2 kikombe Vanilla kijiko 1 JINSI YA KUPIKA 1.Weka sufuria jikoni ikipata moto weka siagi kisha tia sukari koroga tia vanilla ,maziwa ya maji na maziwa mazito kisha koroga kwa dakika 10 usiachie mpaka siagi iyeyuke vizuri kisha epua 2.Paka tray au sinia mafuta kisha mimina mchanganyiko wako,uache kwa dakika 10 kisha weka katika fridge kwa masaa 6 itoe itakua tayari imeganda vizuri katakata vipande weka katika sahani tayari kwa kuliwa.Ni tamuuuu!!! ENJOY! NB: Waweza kuongeza chocolate ukipenda kwa kuikata vipande vipande na kutia katika mchanganyiko wako wakati ushaepua ili chocolate isiyeyuke.
 
Rainbow Cake Keki Ya Upinde Keki Hii huitwa Rainbow Cake Kwa Kuwa Unaweza Tumia Rangi Nyingi Hata Zaidi Ya Mbili. Mahitaji : Unga vikombe 2 Sukari kikombe 1 Mayai 4 Hiliki ya unga kjk 1 cha chai Siagi 1/2 kikombe Rangi ya chakula unayopenda Baking powder kjk 1 cha chai Maelezo : Weka sukari na siagi kwenye bakuli changanya kwa kutumia hand mixer au mwiko mpaka iwe laini. Weka mayai na uchanganye mpaka sukari iyayuke. Weka unga na baking powder, na hiliki ya unga endelea kuchanganya kwa kutumia hand mixer au mwiko kwa dakika 5-7. Gawanya mchanganyiko wa cake mara mbili. Kwenye bakuli 1 weka rangi na mwingine uache hivo hivo. Chukua chombo cha kuokea na uanze kutandaza mchanyiko wako usio na rangi kidogo, Kisha weka mchanganyiko wako wa rangi na umalizie kuweka mchanganyiko usio na rangi Weka kwenye oven kwa dakika 45 hadi lisa limoja. KAMA UNAPIKA KWENYE MAKAA PIKA KAMA UNAPALILIA WALI MOTO WA KIASI JUU NA CHINI. USISAHAU KUPAKA SIAGI KWENYE BAKING PAN YAKO, ILI KEKI ISIWE NGUMU PEMBENI AMA KUKWAMILIA.
 
JINSI YA KUTENGENEZA CHOCOLATE NYUMBANI. MAHITAJI: 🔗Maji 1/2 kikombe 🔗Maziwa ya unga kikombe 1 🔗Siagi 1/2 (unsalted butter) 🔗Sukari kikombe 1 🔗Unga wa cocoa kikombe 1 🔗Vanila kijiko 1 JINSI YA KUPIKA. 1.paka mafuta sinia au tray. 2.Weka maji na sukari ktk sufuria acha ichemke mpaka ukigusa kati ya vidole iwe inanata,kisha weka vanila na siagi ikiyeyuka tia cocoa. 2.Koroga ichanganyike vizuri kisha weka maziwa ya unga kisha anza kusonga kama ugali mwanzoni itakua donge laini songa hadi liwe gumu kiasi kisha mwaga kwenye ile sinia au tray ulioipaka mafuta,itandaze vizuri kisha kata vipande acha ipoe ikisha poa toa vipande weka katika sahani tayari kwa kuliwa. Enjoy
 
HILI NI SOMO AMBALO LIMEENEA SANA SEHEMU NYINGI SANA HIVYO NIMEPENDA KUWALETEA KWA WALE AMBAO HALIJAWAFIKIA🙏 MKAA WA KUTENGENEZA NYUMBANI "Mahitaji" 1.Chenga za mkaa(ule unga unga ) 2.udongo wa kichuguu au mwingne wowote 3.Maji 4.chombo cha kuchanganyia HATUA 1.chukua besen lako weka chenga za mkaa& udongo vichanganye kwa mkon vichanganyikane vzr. 2.Baada ya hapo weka maji kidg kidg kulingana na mchanganyiko wako,mchanganyiko wako usitepete sana uwe wa kawaida 3.Anza kutengeneza maumbo kama ni duara au yai ya size utakayo 4.Anika juani kwa siku 2 au kulingana na ukali wa jua mpaka likauke liwe gum,anika juu ya bati,kwenye karo,jiwe au sehem yoyote ya juu usianike chini. 5.Baada ya hapo tayari kutumia "Jinsi ya kutumia mkaa uliotengeneza" 1.chukua mkaa uliotengeneza utangulize kwenye jiko lako 2.juu yake weka vimikaa kidg vya kupikia kushikishia mabumba yako yakishika hayo ni kama unapikia jiko la gesi Hapo utapunguza gharama ya kununua mkaa kwani utatumia mkaa kdg tu wakati wa kuwasha jiko lako yakishika mabumba yako ndo yanaendeleza upishi wako. Baada ya kujua hilo nimepunguza gharama ya kununua mkaa,kwani mkaa ninaonunua ni kwa ajili ya kuwashia tu si kupikia
 
DONDOO JIKONI: NJIA YA KUHIFADHI NAZI NZIMA ZIKAE MUDA MREFU BILA KUHARIBIKA: chukua mfuko wa unga/sukari utandike chini kisha chukua nazi uziweke juu ya huo mfuko huku ukiwa umeelekeza juu yale macho yake, yaani maji ya nazi yarudi chini na macho yaelekee juu kwani kinachofanya nazi iharibike upesi ni maji yakielekea upande wa macho. njia hii ni rahisi na nzuri sana, kwani inafanya nazi ikae bila kuharibika zaidi ya miezi minne(4)
 
853504368_201704.jpeg
 
Back
Top Bottom