Buns za nyama ndani MAHITAJI: Chumvi vijiko viwili vya chai Sukari vijiko viwili vya chai Amira ya chenga vijiko viwili vya chai Siagi iliyoteyushwa vijiko vinne vya chai Unga wa ngano vikombe vinne Maziwa ya maji ya vuguvugu kikombe kimoja Mayai mawili MAHITAJI YA NYAMA: Nyama ya kusaga yoyote nusu kilo Mafuta ya kupikia vijiko viwili vya chai Tangawizi na kitunguu saumu kilichopondwa kijiko kimoja Soy sauce kijiko kimoja kikubwa ( optional) Maji ya limao au ndimu kijiko kimoja cha chai Nyanya ya pakti vijiko viwili vikubwa Mtindi vijiko viwili vya chai Pilipili manga ya unga nusu kijiko cha chai Chumvi Ufuta vijiko vitatu vikubwa ( kama utapenda) Yai moja JINSI YA KUPIKA: 1) Katika bakuli pana weka maziwa, chumvi, sukari, amira koroga vichanganyike na uache kwa dk 10 kisha mimina siagi na vunjia mayai na tumia mchapio au hand mixer kuchanganya mpaka vichanganyike 2) Halafu anza kuweka unga weka kikombe kimoja kimoja huku unaendelea kuchanganya upate donge kanda lilainike kisha funika kwa saa moja liumuke 3) Chukuwa nyama yako ya kusaga weka katika bakuli kisha weka soy sauce, maji ya limao au ndimu, chumvi, mtindi, pilipili manga , tangawizi na kitunguu saumu kisha changanya na uifunike kwa nusu saa 4) Baada ya nusu saa weka pan jikoni weka mafuta yakipata moto kiasi mimina nyama yote na anza kuigeuza geuza ikianza kukauka maji weka nyanya na endelea kuipika mpaka iwe kavu iive kisha epua 5) Chukuwa unga wako ulioukanda ukaumuka anza kukata madonge, kisha chukuwa donge moja tumia vidole kulisukuma upata nafasi ya kuweka nyama kisha weka nyama ya kutosha na ufunge donge lako vizuri kama tunavyofanya katika chapati za kusukuma fanya hivyo madonge yote yaishe kisha yapange katika trey la oven acha nafasi kati ya donge moja na lingine ili yapate nafasi wakati wa kuoka yafunike tena kwa nusu saa 6) Baada ya nusu saa Chukuwa yai moja weka katika bakuli na maji kidogo lipige kisha Pakaa juu ya madonge yako na unyunyizie ufuta juu ya madonge yote 7) pre heat oven kwa dk 30 katika moto wa 200C halafu uoke -