BAADHI YA VIUNGO, MATUMIZI NA FAIDA ZAKE -> Kitunguu saumu (Garlic) Kitunguu saumu ni kiungo ambacho kimekuwa maarufu kwa matumizi mbalimbali. Vipo vitunguu saumu vya rangi nyeupe ambavyo mara nyingi huwa na tumba kubwa ambazo ni chache. Vingine ni vile vyenye rangi ya zambarau au pinki ambavyo huwa na tumba ndogo na nyingi. Vitunguu hivi vina ubora sawa. Kitunguu saumu hufaa katika matatizo mengi kama kusaidia kuzuia maambukizi yatokanayo katika utumbo, mapafu na sehemu za ukeni. Vilevile husaidia katika uyeyushwaji wa chakula, kuzuia kuharisha na pia hupunguza fangasi za kinywani, maambukizi katika koo na hata mkanda wa jeshi. Kitunguu saumu kinaweza kutumika katika mapishi ya chakula, chai au kinywaji chochote cha baridi au cha moto. Mtu anapotumia vitunguu saumu atumie kwa kiasi. Inashauriwa kutumia vitumba visivyozidi sita kwa siku hasa kama vitatumika vibichi . -