Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mourinho na Spurs yake atahitaji kushinda ili kusogea kwenye Top Four inayotoa tiketi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini Klopp kikosi chake kipo kwenye mwendo wa kutisha kikiwa na dhamira moja ya kuelekea kuvunja rekodi ya Arsenal ya kucheza msimu bila ya kupoteza.
 
Rekodi pia zinambeba Klopp, ambapo kwenye mechi 10 zilizopita alizocheza dhidi ya Mourinho, Mjerumani huyo amepoteza mechi mbili tu, huku safari hii Mourinho akienda kumkabili mpinzani wake huyo akiwa na majeraha kibao kwenye kikosi chake akiwamo straika wake namba moja, Harry Kane.
 
Manchester United nayo ina shughuli mbele ya Norwich City. Tangu mwaka huu, 2020 uingie, kikosi hicho cha Ole Gunnar Solskjaer hakijashinda, huku kikifanikiwa kupata bao moja tu katika kipigo cha 3-1 kutoka kwa Manchester City kwenye Kombe la Ligi.
 
Back
Top Bottom