TABIA njema ni kitu kinachoweza kuongeza thamani na amani katika ndoa. Ila kwa sababu za kitaalamu sijawahi kumshauri mtu aoe ama aolewe kwa kigezo cha tabia njema pekee.
Tathmini na uzoefu unaonesha mtu anaweza kuwa na tabia njema ikiwa tu anakupenda na kuamini wewe ni mtu wa thamani katika maisha yake. Mtu akupendaye kwa dhati ataogopa kukupoteza na kwa kigezo hicho atajikuta anakuwa mtulivu, makini na mwerevu kadiri iwezekanavyo ili akufanye ujihisi uko na mtu sahihi katika maisha yako.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.