Manchester United itajaribu kupata saini ya mchezaji wa kimataifa wa Uingereza na klabu ya Birmingham mwenye umri wa miaka 17 Jude Bellingham wakati wa majira ya joto baada ya kuwa waliweka dau la paundi milioni 20 wakati wa dirisha dogo la usajili. (Independent).
Wakala wa mchezaji wa kimataifa wa Nigeria, Odion Ighalo alizungumza kwa siku kadhaa na afisa mtendaji wa klabu ya Manchester United, Ed Woodward kabla ya mchezaji wake mwenye umri wa miaka 30 kukamilisha usajili wa siku ya mwisho. (Aftenposten, via Express).
Ighalo aliduwaa kwa uamuzi wa klabu ya Manchester United kuamua kumsajili katika dakika za lala salama licha ya kuwa hakukuwa kunaonekana kuwepo kwa uwezekano. (Mail).
Beki wa zamani wa Manchester United, Gary Neville amesema anaamini usajili wa Ighalo umeonesha utaratibu mbovu wa usajili uliopo kwenye klabuj hiyo. (Sky Sports).