Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Lakini kuhusu dawa za kuzuia kubeba mimba katika kipindi hiki, mnashauriwa muwe na tahadhari kuhusu kutumia njia yoyote itayoathiri mfumo wa homoni. Hii ni kwa sababu itaathiri sana kiwango na ubora wa maziwa na itamsababishia mtoto kutopata lishe inayotakiwa.
 
Shirika la Afya Duniani linasisitiza mtoto anywe maziwa tu kwa muda usiopungua miezi 6 kisha uendelee kumnyonyesha mpaka atakapofikisha miaka miwili. Wazazi wengi wanaona hii inawatesa na wengi wao wanasema kwamba miezi 6 ya mwanzo ni muhimu sana.
 
Unashauriwa uzungumze na daktari wako kuhusu muda gani unaweza kurudia kufanya mapenzi na njia za kutumia kujikinga na mimba ya haraka na pia umuulize hasa kuhusu kutumia dawa zenye progesterone na madhara yake kwako. Vidonge hivi vinaathiri maziwa (kwa wingi na ubora) kwa kiwango kidogo zaidi ukilinganisha na vidonge vyenye oestrogen.
 
Mwili wako umefanya kazi kubwa sana ya kuleta kiumbe duniani. Sio tu kwa sababu ni utambulisho wako na kukufanya uitwe ‘mama’ na chochote utachofanya kitakachokufurahisha, utashangaa jinsi ulivyo na sehemu nyingi zinazoweza kukufanya upate raha.
 
Kuna ukweli.??
IMG-20200202-WA0007.jpeg
 
Back
Top Bottom