Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Andreas Pereira ni mchezaji mwingine atakayeelekea kwenye mlango wa kutokea, ambapo bila ya shaka usajili wa mastaa wapya kama Grealish na Maddison ukikamilika, basi Pereira hatakuwa na nafasi kwenye timu ikiwa msimu huu amefunga mara moja tu katika mechi 23 alizocheza kwenye ligi.
 
Mchezaji wa tano kutajwa kwenye orodha hiyo ni beki wa kati, Phil Jones. Beki huyo amekuwapo Man United tangu enzi za Sir Alex Ferguson, lakini kiwango chake kimeonekanna kushuka sana kwa siku za karibuni na kuonekana hana anachoweza kukifanya kwenye timu tena akiwa amecheza mechi mbili kwenye Ligi Kuu England msimu huu.
 
SI umesikia mlipuko wa kirusi cha corona? Ugonjwa uIlioanza kuitesa China na sasa unaonekana kusambaa katika nchi kadhaa duniani, basi kama hautamalizwa kwa wakati utaivuruga michuano ya Euro 2020 na matukio kadhaa ya michezo ulimwengini.
 
Euro 2020

Itafanyika katika viwanja 12 tofauti barani Ulaya kati ya Juni 12 hadi Julai 12, 2020, huku fainali yake ikitarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Wembley, London, England, huku mechi ya ufunguzi Juni 12, jijini Roma ikizikutanisha Italia na Uturuki.
 
Tuko katika hali ya kusubiri. Tunazifuatilia nchi zote na soka lazima tufuate taratibu za nchi husika,” anasema Michele Uva, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya UEFA. “Ishu za michezo zitalazimika kusimama kama hali ikiwa mbaya.”
 
Wakati wa maandalizi ya mechi ya juzi Jumatano Ligi ya Mabingwa Ulaya ambayo Olympique Lyon iliichapa Juventus bao 1-0, ulitokea mvutano ambapo baadhi ya wanasiasa wa Ufaransa walitaka mashabiki wa Juve wazuiwe kuingia Ufaransa kwa hofu ya Corona.
 
Lakini Kocha wa Juventus, Maurizio Sarri alipingana na hilo na kutetea mashabiki wake na kusisitiza wana haki ya kuiona timu yao ikipambana Ulaya, Japokuwa mwisho waliruhusiwa kuingia Ufafansa na kuiona timu yao, ila unaweza kuona hofu ilivyo kubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…