Nashukuru kiasi furani umeenda sawa.
Ilikuwa hivi.
Simba ilikuwa na mfadhili aitwaye Azim Dewji.
Wakati tunaingia kwenye mashindano hayo kombe la CAF, Azim Dewji aliwaweka kitako wachazaji, akaawaambia kwamba kutoka kwenye mgao wao wa mapato ya mlangoni (viingilio) atamfungulia kila mmoja account, kwa hiyo kila mmoja fungu lake litawekwa hapo, kwamba wajitahidi mpaka wachukue Ubingwa.
Wakichukua ubingwa atawaongezea na hivyo kila mmoja atamnunulia gari pick up aina ya KIA. Gari hizo wakati huo zilikuwa maarufu kwa usafiri wa daladala, ziliitwa jina la utani "Chai Maharage"
Ahadi ilitolewa baada ya mechi ya kwanza.
Mechi ya kwanza ilichezwa jijini Mwanza na Freviaro ya Msumbiji.
Baadaye tukaitoa Mbabane Highlanders ya Swaziland na kisha USMA al Harrach ya Algeria na baadaye Sportivo Klabu Aviacao.
Baada kuitoa Avicao ya Angola ambayo ilisifika sana wakati huo, hasa wachezaji wake kama Abilio, Lidenge, Kalekiwa Kaleki, na hasa hasa golikipa wao Kanka Wemba aliyekuwa raia wa Zaire.
Golikipa huyo alisifika kwa uwezo wake lakini iliwachukua Simba dakika sita tu kumfunga goli la kwanza kwa goli la Edward Chumila.
Aviacao walifungwa bao 3-1, Dsm.
Mechi ya maridhiano nchini Angola iliisha kwa sare ya 0-0.
Simba walicheza fainali na Stella Abidjan ya Ivory Coast.
Kwenye mechi ya kwanza ya fainali iliyochezwa jijini Abidjan matokeo yalikuwa 0-0.
Mechi ya pili iliyochezwa uwanja wa taifa kwa sasa uhuru Simba ilifungwa goli 2-0.
Magoli yote yalifungwa na Boli Zozo.
Kikosi cha Simba kilikuwa cha wazawa watupu.
1.Mwameja Mohamed (Tanga)
2.Kasongo Athumani (Tanga)
3.Deo Mkuki (Mwanza)
4. Godwin Aswile (Mbeya)
5.George Masatu (Mara)
6. Hussein Marsha. (Mwanza)
7.Abdul Mashine. (Dsm)
8. Ramadhani Leny, (Rukwa)
9.Edward Chumila. (Moro)
10. Malota Soma (Moro)
11. Thomas Kipese. (Dsm)
Sub.
12.Often Martin (Mbeya)
13.Rashidi Abdaalah (Mwanza)
14. Fikiri Magoso (Moro)
15.Iddi Selemani (Dsm)
16. Damian Kimti
17. Razak Yusuf (Tanga)
Kocha Abdallah Kibaden "King"
Sent using
Jamii Forums mobile app