Davet
JF-Expert Member
- Apr 5, 2013
- 42,474
- 206,022
😀😀😀😀 huyo baharia katisha sana ila nikweli huu ukamiaji sio safi hasa kwa hawa watoto wazuri mixer ushombe shombe, usipokuwa makini unashusha heshima ya ukooKukamia ndo mwanzo wa kuchemsha....
Kuna uzi ule wa mabaharia walikuwa wanaelezana shoo mbovu walizowahi kupafomu. Baharia mmoja akafunguka eti alikuwa kamkamia demu pini kali hatari siku ya siku demu kazuka ghetto sasa eti ile tu anapishana naye mlangoni wakagusana basi baharia wareno haooo...na Abdallah kichwa hakuamka tena. Nilicheka sana aisee lakini ndo hivyo mkamia maji hayanywi. Hata ukijipigilia hizi alkasusu zenu kama umekamia sana waweza ishia kuchemsha unabubujika hovyo hovyo tu bila mpangilio [emoji16][emoji16][emoji2221][emoji2221]
Kijana alikuwa bado hajazaliwa Bro.. Ongezea Simba hiyo iliyokuwa bora kwa kila idara ilifanikiwa kufika fainali ya Kombe la washindi barani Africa sasa hv linaitwa Kombe la shirikisho, na kwenye mchezo wa fainali ilikutana na timu moja toka Ivory Coast..
Kabla ya fainali hii wachezaji wa Simba waliahidiwa kila mchezaji kupewa gari(nmesahau aina ya gari, ni miaka mingi imepita, uzee huu)
Mwisho wa siku Simba ilipoteza kwenye fainai iliyopigwa kwenye dimba la taifa na kikubwa zaidi wanadai ilifanyika hujuma kwani Simba ile kubeba ubingwa ilikuwa ni kawaida tu sema ndio hvyo Boss wa Simba wakat ule alijistukia kutoa ile zawadi kwa hyo Simba ikapoteza ile game...
Hahah! Bro 93 zamani sana sikumbuki kama nilikua na umri ila huu mjadala wetu naona kabisa hatumalizi leo wala kesho acha nitafute siku nije TMK tubadilishane mawazo vizuri
🙌🙌🙌 bro upo vizuriNashukuru kiasi furani umeenda sawa.
Ilikuwa hivi.
Simba ilikuwa na mfadhili aitwaye Azim Dewji.
Wakati tunaingia kwenye mashindano hayo kombe la CAF, Azim Dewji aliwaweka kitako wachazaji, akaawaambia kwamba kutoka kwenye mgao wao wa mapato ya mlangoni (viingilio) atamfungulia kila mmoja account, kwa hiyo kila mmoja fungu lake litawekwa hapo, kwamba wajitahidi mpaka wachukue Ubingwa.
Wakichukua ubingwa atawaongezea na hivyo kila mmoja atamnunulia gari pick up aina ya KIA. Gari hizo wakati huo zilikuwa maarufu kwa usafiri wa daladala, ziliitwa jina la utani "Chai Maharage"
Ahadi ilitolewa baada ya mechi ya kwanza.
Mechi ya kwanza ilichezwa jijini Mwanza na Freviaro ya Msumbiji.
Baadaye tukaitoa Mbabane Highlanders ya Swaziland na kisha USMA al Harrach ya Algeria na baadaye Sportivo Klabu Aviacao.
Baada kuitoa Avicao ya Angola ambayo ilisifika sana wakati huo, hasa wachezaji wake kama Abilio, Lidenge, Kalekiwa Kaleki, na hasa hasa golikipa wao Kanka Wemba aliyekuwa raia wa Zaire.
Golikipa huyo alisifika kwa uwezo wake lakini iliwachukua Simba dakika sita tu kumfunga goli la kwanza kwa goli la Edward Chumila.
Aviacao walifungwa bao 3-1, Dsm.
Mechi ya maridhiano nchini Angola iliisha kwa sare ya 0-0.
Simba walicheza fainali na Stella Abidjan ya Ivory Coast.
Kwenye mechi ya kwanza ya fainali iliyochezwa jijini Abidjan matokeo yalikuwa 0-0.
Mechi ya pili iliyochezwa uwanja wa taifa kwa sasa uhuru Simba ilifungwa goli 2-0.
Magoli yote yalifungwa na Boli Zozo.
Kikosi cha Simba kilikuwa cha wazawa watupu.
1.Mwameja Mohamed (Tanga)
2.Kasongo Athumani (Tanga)
3.Deo Mkuki (Mwanza)
4. Godwin Aswile (Mbeya)
5.George Masatu (Mara)
6. Hussein Marsha. (Mwanza)
7.Abdul Mashine. (Dsm)
8. Ramadhani Leny, (Rukwa)
9.Edward Chumila. (Moro)
10. Malota Soma (Moro)
11. Thomas Kipese. (Dsm)
Sub.
12.Often Martin (Mbeya)
13.Rashidi Abdaalah (Mwanza)
14. Fikiri Magoso (Moro)
15.Iddi Selemani (Dsm)
16. Damian Kimti
17. Razak Yusuf (Tanga)
Kocha Abdallah Kibaden "King"
Sent using Jamii Forums mobile app
Nakumbuka bro..... hapo mgeni Rasmi kwenye hiyo game alikua ni Rais wa Jamuhuri ya muungano enzi hizo mzee Ally Hassan Mwinyi, na hapo ndipo ile kauli ya Tanzania Kichwa cha mwendawazimu ilianzia baada ya kukosa lile kombe Rais Mwinyi alitoa hiyo kauli....
Simba kilicho waangusha kwenye ile game ni imani za kishirikina maana usiku kabla ya game wachezaji hawakulala usiku kucha walikua wanapikwa, hiyo ilisababisha uchovu wa wachezaji siku ya mechi.
Umenikumbusha mbali mzee mwenzangu maana siku hiyo nilikua pale Shamba la bibi nikishuhudia mtanange live bila chenga
Hatari sana bro, hakika hii ni siku ya kukumbukwa nchini hasa katika tasnia ya michezoSimba baada kupata Sare jijini Mwanza walipocheza mchezo wao wa awali, wakahamia uwanja wa nyumbani taifa kwa mechi zao zote.
Kuanzia hapo Uwanja huo ulikuwa ni machinjio
Mbabane walifungwa bao 1-0.
Kwao pia walifungwa 0 - 1.
USMA al Harrach 3-0
Kwao walishinda 2-0
Aviacao walifungwa 3-1
Kwao 0-0
Kuanzia hapo Simba na mashabiki wake walijenga imani kwamba ukikanyaga uwanja wa taifa umekwisha.
Na tangu mashindano hayo yameanza Simba ilianza mechi zake zote nyumbani ila mechi ya mwisho ya fainal ya kwanza.
Simba ilipata sare ya 0-0 kwenye fainali ya kwanza Abidjan tena ikicheza na wachezaji wa akiba baada ya kuwakosa wachezaji 5 wa kikosi cha kwanza kutokana na sababu mbalimbali.
Baada ya sare hiyo ya ugenini jiji la Dar lilikuwa kwenye tahatuki ya Ubingwa maana kila mmoja aliamini Simba lazima itashinda fainali ya mwisho kwa kuwa tunamalizia nyumbani na hakuna timu iliyowahi kupata salama kwenye uwanja wa nyumbani wa Simba.
Kazi ilianzia hapo.
Taharuki hiyo iliifanya serikali iunde kamati ya ushindi iliyokuwa na wajumbe toka wizara utamaduni na michezo, polisi na FAT ( TFF ya wakati huo).
Siku ya Fainali serikali yote ya Tanzania ilihamia uwanja wa taifa, rais, makamo wa rais na Waziri Mkuu na Mawaziri karibia wote.Rais wa Zanzibar na baadhi ya Mawaziri wake.
Bro kwa kifupi kila mmoja alitamani afike ajionee kwa jicho lake namna Simba inavyoandika historia
Mpaka kufikia saa 5 asubuhi siku ya mechi uwanja ulifungwa maana ulijaa kupita kiasi.
Kwahiyo nadhani kilichotughalimu siku hiyo ni kujiamini kupita kiasi
Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]SIMBA kama mnaona YANGA wanafaidika saana na BENARD MORRISON na nyie msajilini BENARD MEMBE yupo huru sasa hivi 🤣🤣🤣