Kichwa cha mwendawazimu hakikuanzia hapo.
Mwaka 1986 kwenye ufunguzi wa mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na kati.
Mashindano hayo yalifanyika Tanzania na mwenyeji akiwakilishwa na Yanga.
Ikumbukwe Tanzania ilikuwa ndiyo nchi ya kwanza kwa timu yake ya Simba kubeba Kombe hilo kwa mara ya kwanza mwaka 1974 na baadaye Yanga mwaka uliofuata.
Kuanzia hapo Tanzania ilipotea kabisa kwenye mashindano yote ya kimataifa.
Kwahiyo kwenye uzinduzi huo Mwinyi akiwa na mwaka madarakani aliwaonya viongozi wa FAT na michezo mingine wasiifanye Tanzania kuwa kichwa cha mwendawazimu ambacho kila mlevi anajifunzia kunyoa.
Ujumbe huo ulifanya Yanga ipambane kufa na kupona mpaka ikafika fainali.
Na baada kufungwa bao 2-0 mpaka dakika 75 na el Mereikh ya Sudani, Yanga kupitia kwa mchezaji wake chipukizi wakati huo Abubakar Salum "sure boy" ilisawazisha mabao yote na kuja kupoteza mchezo kwa penati.
Mwaka 1991 Simba ilishinda kombe hilo.
Rais mzee Mwinyi aliwaalika Ikulu kula nao chakula cha mchana na kisha akasema "kuanzia leo nafuta kauli yangu ya Tanzania kuwa kichwa cha mwendawazimu" hiyo ilikuwa ni 1991 bro.
Na mwaka uliofuta 1992 Simba ilitetea Ubingwa wake kwa kuifunga Yanga kwenye fainali ya kukata na shoka iliyopigwa Uwanja wa Amani Zanzubar
Upo vizuri kumbe, nisamehe mzee kwa hilo...umri umetutupa mkono.
Kweli kabsa kichwa cha mwendawazimu kilianzia hapo..
Dah, umenikumbusha mbali kweli mzee mwenzangu, wakati wa fainali hii ndio naingia mjini kwa kudandia yale ma FIYAT..