Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mbinu bomba sana ila inakera[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hahahah! Walinishangaza sana vile jamaa walijipanga kuzuia ile free kick sikujua kama ni mbinu inazinduliwa 😂😂😂

Kuna hii nyingine ilizinduliwaga ya wachezaji wengine kulala chini ya ukuta ili kuzuia asipitishe mipira chini ya miguu
 
Nikwambie tu bro, Abdalallah Kibani ndiye kocha mwenye mafanikio mengi kuliko makocha wote waliofanya kazi Tanzania.
Bahati mbaya tu kwamba hatupendi kuthamini watu wetu kama kauli maarufu isemaye 'Nabii hakubaliki kwao" .
[emoji119][emoji119][emoji119] bro upo vizuri

Kibadeni King Mungu azidi kumbariki huyu mzee, alikuwa kocha wangu pale JKT Tanzania kwenye kikosi cha Under 20
 
Niliamua kufanya udadisi kujua kinywaji hicho cha Al Kasusu ni kitu gani, kwani siku moja nikiwa ofisini nilisikia baadhi ya wafanyakazi, wakibishana kuhusu kinywaji hicho, na baadhi walisema ni cha kuongeza nguvu za kiume na ndio kinywaji maarufu hivi sasa mjini.
 
Kijiwe cha Mtoni Mtongani Kijiwe hiki kipo nyuma ya kituo cha mabasi yanayoelekea njia ya Mbagala, ambako hapa ni zaidi inauzwa kahawa huku wateja wengi ni watu wa rika la kati na watu wazima. Kuna mabirika mengi kidogo, huku wanywaji wakitumia muda wao mwingi kunywa na kuzungumza masuala mbalimbali.
 
Baada ya kunywa nusu kikombe cha Al Kasusu, iliyokuwa ikinywewa kwa kiasi kikubwa na watu waliokuwa kwenye eneo hilo, nikagundua ni kinywaji chenye ladha ya kahawa, maziwa na sukari kwa mbali, lakini ukiinywa unabainisha kuwa kuna kitu cha nyongeza.
 
Niliamua kuvunja ukimya kwa kuzungumza na muuzaji wa kinywaji hicho, Ali Mzee ambaye bila kusita alibainisha kuwa kinywaji hicho kinatengenezwa kwa maziwa, unga na kahawa kidogo. Nikajikuta ninavutiwa zaidi kufahamu kuhusu unga huo, ambao unachanganywa.
 
Kuhusu undani kama Al Kasusu ni kweli inasaidia kama alivyodai muuzaji wake, mmoja kati ya watumiaji waliozungumza na gazeti hili, alibainisha kuwa kwa upande wake ilimsaidia siku ya kwanza alipoitumia, lakini haoni kama inamsaidia zaidi, isipokuwa yupo kwenye uwezo wake wa kawaida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…