Waziri huyo amepata maambukizi ikiwa tayari watu sita wameripotiwa kufariki dunia nchi humo na visa 382 vinavyotokana na ugonjwa huo vikiwa vimeripotiwa.
Katika jitihada hizo, mamlaka hizo zimesema kuwa baada ya kufanya maboresho zitaweza kufanya vipimo vya watu 10,000 kwa siku tofauti na sasa ambapo watu 1,500 hupimwa kwa siku.
Pia wamesema kuwa watahakikisha majibu ya vipimo yanatoka ndani ya saa 24
Katika taarifa yake, waziri huyo ambaye pia ni mbunge wa Bedfordshire amesema kuwa idara ya afya imeanza kuwafuatilia watu waliokuwa karibu naye, na ofisi yake ya bunge inafuatilia hilo kwa karibu.
Kocha wa Tottenham Spurs, José Mourinho amesema kikosi chake kinawakati mgumu msimu ujao kushiriki katika Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuondolewa na RB Leipzig ya Ujerumani kwa jumla ya mabao 4-0.
Spurs katika mchezo wa kwanza nchini England walipoteza kwa bao 1-0, walishindwa kufua dafu katika mchezo wa marudiano mbele ya Leipzig kwa kukubali kipigo cha mabao 3-0 kwenye uwanja wa Red Bull Arena.
“Kwa kikosi nilichonacho katika kipindi hiki ni ngumu mno,” alisema Mourinho. “Kibaya zaidi ni kwamba tatizo letu haliwezi kumalizika leo wala kesho, lakini tutapambana hadi mwisho.
“Upande wa Ligi Kuu England tumekuwa tukipata matokeo tofauti na yale ambayo tumekuwa tukiyahitaji. Tumepoteza 3-2, 2-1, 1-0 haina maana kuwa hatotoendelee kupambana,” alisema kocha huyo mwenye maneno mengi.
Spurs katika michezo iliyopita iliwakosa wachezaji wao muhimu wakiwemo, Steven Bergwijn, Ben Davies, Harry Kane, Davinson Sánchez, Moussa Sissoko na Son Heung-min kutokana na kusumbuliwa kwao na majeruhi.