Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mwanamke huyu mzaliwa wa Ghana ambaye kwasasa anaishi Walsall, Birmingham Uingereza aligunduliwa akiwa na hali hiyo miaka mitano baada ya kujifungua mtoto wake Rashley ikiwa ni zaidi ya miaka 21 ya kwenda na kurudi hospitali bila kugundulika tatizo lake.
 
Elizabeth amekuwa akisumbuliwa sana na Tumbo hususan akiwa katika siku zake za mwezi hali iliyokuwa ikimpelekea mpaka kupoteza fahamu huku kwa muda mrefu na katika hospitali tofauti tofauti akiambiwa kuwa ana tatizo la mayoma hivyo hatoweza hata kupata mtoto.
 
Safari ya miezi tisa haikuwa rahisi kwake kwani katika kipindi cha ujauzito alikabiliwa na utokaji wa damu sana, kupoteza fahamu na uchovu usiomithilika. “Ulikuwa ni ujauzito wa changamoto kubwa, nilikuwa natokwa na damu muda wote, uchovu mwingi na wakati mwengine nilikua napoteza fahamu” anaeleza Elizabeth
 
Madaktari walidhani ujauzito umetunga nje ya fuko la uzazi kwasababu sote hatukujua kama nina mafuko mawili”. Anafafanua Elizabeth. “Pia nilipokuwa nikifanyiwa skanning kutizama maendeleo ya mtoto tumboni wakati mwengine walimuona na wakati mwengine hawakukuta kitu kwasababu walitizama kwenye fuko tofauti na alilokwepo mtoto na hawakuweza kudhani kuwa nina mafuko mawili kutokana kwamba si kawaida kutokea tatizo hili”
 
Mwaka 2015 kipimo cha MRI kilionesha kwamba Elizabeth ana mafuko mawili ya uzazi. “Ilinishangaza kwani sikuwahi kusikia kuwa kuna mtu ana mafuko mawili ya uzazi na mwaka 2016 walinifanyia upasuaji na kugundua pia ni njia mbili za uzazi na sehemu mbili za uke”
 
Wakati mbappe anaibuka watu walikua na huu msemo wa kutomuweka rum moja na ronaldo au messi ila haland anaweza fika mbali kama hatatawaliwa sana na meneja wake. Cheki pogba nowdays story juu yake kwisha
Mbappe still hajakaa room moja na hao wakina Ronaldo, ila Haaland kufikia wakina Mbappe inawezekana kwasababu wale ni upper middle class players kinachohitajika ni muda na matunzo kama ulivyosema.....

Story ya Pogba kwakweli inasikitisha mana nilishamsahau 😀
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…