Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Elysia chlorotica ndiyo mnyama pekee anayeweza kujitengenezea chakula chake mwenyewe kama mmea. Mnyama huyo anayepatikana kwenye bahati ya Atlantic ana chembeumbijani (chroloplasts) anazozipata kwa kula mimea na kisha anazitumia kujitengenezea chakula. (National Geographic)
 
Umri ambao mtu anaanza kufanya mapenzi unaweza kusababishwa na vinasaba alivyorithi kutoka kwa wazazi wake. 25% ya watu hufanya ngono kwa mara ya kwanza katika umri sawa na ambao ndugu zao wengine walianza. (TheGuardian)
 
Mvi' hutokea baada ya seli zinazotengeneza rangi ya nywele kuchoka au kufa. Kupata mvi katika umri mdogo huitwa "Canities" hutokana na muingiliano wa jini (gene) za urithi, mazingira na lishe.
 
Simu ya kwanza ilitengenezwa na Alexander Graham Bell mwaka 1876. Mpaka anafariki alikataa kabisa kutumia simu sababu akitaja ni kuweka umakini zaidi katika kazi zake, hivyo kutumia simu ingemchanganya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…