Miaka ya 1990's, Michael Jackson alitaka kuinunua kampuni ya Marvel ili apate nafasi ya kuigiza uhusika wa Spider-Man. MJ alikuwa ni shabiki mkubwa wa uhusika huo.
Ndoa za kisukuma zinaruhusu ndoa za mitaala(mke zaidi ya mmoja).
Kwa kawaida wasukuma huoa kwa mahali ya ng'ombe kati ya 7 mpaka 20. Hii ni kawaida lakini mahari inaweza kuwa ng'ombe 25 mpaka 70 pale atakapokuwa anaozeshwa Binti mweupe.
Wanasayansi katika tafiti huepuka kuwatumia watu wanaotumia mashoto kwa sababu ubongo wao unafanya kazi tofauti na watu wanaotumia kulia hivyo huogopa kupata majibu ambayo yanaweza kuleta madhara baadae.
Hamar' ni kabila lingine kutoka Ethiopia, hawa wana utamaduni ambapo binti ambae anajiandaa kwaajili ya kuolewa hutakiwa kujipaka udongo mwekundu mwili mzima na hatakiwi kuoga kwa kwa zaidi ya miezi 03. Hufanya hivyo kwaajili ya kujiandaa na majukumu ya ndoa.
Kabila la Mursi linapatikana nchini Ethiopia, Kwa Wanawake hupenda kuweka bakuli katika midomo yao ambayo hufikia urefu mpaka sentimeta 20. Ukubwa wa bakuli utavyokaa mdomoni huongeza mvuto zaidi (Wanavyoamini wao). Utaratibu huo ulianza kipindi cha ukoloni ambapo walikuwa wakifanya hivyo ili kuzuia kuchukuliwa kama watumwa lakini kwa sasa ni urembo
Tafiti: Watoto nchini Ufaransa hulia kwa sauti ya juu, Ujerumani hulia kwa sauti ya chini sababu inatajwa ni kutokana na Lugha ambazo huanza kuzisikia tangu wakiwa tumboni mwa Mama.Watoto wa Tanzania 🤔?
Sonona (Depression) inaambukiza. Ukitumia muda mwingi kukaa na mtu ambae anasumbuliwa na Msongo wa mawazo uliopitiliza (Depression) inaweza kupelekea na wewe pia kuanza kusumbuliwa na tatizo hilo.
Mrs Feodol vasslyev alizaliwa mwaka 1707 shurya nchini Urusi huyu ni mwanamke aliyeshika rekodi ya kuzaa watoto wengi zaidi duniani watoto 69 na ameingia kwenye kitabu cha rekodi za dunia GUINNESSAlizaa mapacha wawili Mara 16, watatu ×7 na wanne ×4
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.