Area 51' ni eneo Marekani linalopatikana huko Nevada ambalo linatajwa kuwa ni maalum kwaajili ya kuandaa, mafunzo na kufanyia majaribio vifaa vya anga vya kijeshi. Vitu vingine vinavyoendelea havifahamiki japo kuna taarifa zinazosambaa kuwa ni eneo ambalo wanatumia kuwasiliana na Alien' na kuna watu kadhaa ambao wanasema wamewahi kufanya kazi hapo, wanakiri kufanya kazi na Alien kadhaa. Hakuna uthibitisho wowote sababu eneo hilo shughuli nyingi ni za siri sana.