Ushawahi Kujiuliza Mitandao Kama Facebook, Twitter, Instagram, WhatsApp, Google na mingineyo inapata vipi Pesa?.
Mitandao Mingi Ya Kijamii Namna Inavyopata Pesa Ni Kama Mfumo Wa Radio Na Tv Stations Au Media Zingine Ambazo Zinakuwa Zimeamua Kutoa Huduma Zao Bure Kwa Jamii.
Kwamba Wanachofanya Ni Kukusanya Watu Wengi, Kisha Katika Hao Watu Wengi Ndipo Huwashawishi Makampuni Mbalimbali Kuweza Kutangaza Sababu Kuu Ni Uwepo Wa Watu Sababu Kila Siku Makampuni Yanahitaji Kutangaza Na Yanahitaji Watu Na Hayataacha Kutangaza...Hapa Utakutana Na Hizi Media Zinatengeneza Kitu Kinaitwa Rate Card.
Sasa Kwa Mitandao Ya Kijamii Walichofanya Ni Kutoa Huduma Bure Kwa Watu, Utoaji Wa Huduma Bure Umesababisha Uwepo Wa Watu Wengi Ambao Umepelekea Makampuni Mbalimbali Kuanza Kuweka Matangazo Yao Hasa Kutokana Na Uwepo Wa Watu Wengi.
Hapo Ndiyo Tunakutana Mfano Instagram, Facebook na Mfumo Wao Wa Matangazo Ya Sponsored Ads' Ambapo Unawalipa Na Wao Wanakuwekea Tangazo Lako Kutokana Na Gharama Uliyoweka Na Watu Wangapi Iwafikie.
Kingine Kuna Njia Inaitwa Mining Data' Hii Wanaitumia Sana Google Lakini Facebook Ndiyo Kashfa Iliwakuta Majuzi Hasa Katika Uchaguzi Wa Marekani, Kwamba Haya Makampuni Yanauza Taarifa Zako Kwa Makampuni Mbalimbali.
Hapa Nitakupa Mfano Mdogo, Ushawahi Ona Mfano Kama Unapenda Kuperuzi Kuhusu Kutafuta Ajira Katika Google Au Yoututube Basi Unaanza Kuona Hata Matangazo Ambayo Wanakuletea Ukiwa Katika Webs Mbalimbali Ni Yanahusu Ajira?
Ukiona Hivyo Jua Taarifa Zako Zimeuzwa...Pia Njia Nyingine Wanapata Pesa Kupitia Vifurushi Vya Data Unavyonunua Japo Hii Sio Njia Kubwa Wanayopata Kipato.
Hapa Wanalipwa Na Wanaotengeneza Mfumo Wa Matumizi Ya Intaneti Tunawaita ISP (Internet Service Provider) Ambapo Kama Utatumia Mfano Data Yako Kwa Kiasi Kikubwa Kuperuzi Facebook, Youtube, Instagram Etc
Kile Kiasi Ulichotumia Kuna Makato Ambayo Huingia Kwenye Kampuni Husika (Facebook, Youtube N.K) Sababu Inakuwa Kwa Kiasi Kikubwa Wamekusaidia Kummalizia Mtu Bando Lake La Intaneti.
Hizo Ndiyo Njia Kadhaa Zinazofahamika Kwa Urahisi, Kama Unaijua Nyingine Unaweza Kuongezea, Asante!