Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hii inaumiza sana maana nafasi kama hizi huwa haziji mara mbili, huu ulikuwa wakati wa wachezaji wengi wa Liverpool kuvaa medali ya Ligi Kuu kwa mara ya kwanza na kufanya kile kilichomshinda Gerrard, lakini ndiyo hivyo majanga yanataka kuwaharibia. Na ndoto yao ya kuvaa medali katika maisha yao ya soka ikafia hapa.
 
1. Antoine GriezmanUmri: Miaka 28Klabu alizochezea: Real Sociedad, Atletico Madrid, BarcelonaMechi za Ligi: 386Mfaransa huyu ambaye aliwahi kupita kwenye kikosi cha Real Sociedad mwaka 2014 kabla ya kutua Atletico Madrid, sasa anakipiga katika klabu ya Barcelona. Kote huko amecheza jumla ya mechi 386, lakini pamoja na ubora wake hajawahi kutwaa taji la Ligi Kuu katika nchi alizocheza.
 
2. Marco ReusUmri: Miaka 30Timu alizocheza: Rot Weiss Ahlen, Borussia Monchengladbach, Borussia DortmundMechi za Ligi: 328Amekuwa na mahaba makubwa na vitanda vya hospitali iliyojengwa na viingilio vya dimba la Signal Iduna Park, kwa kuwa amekuwa rafiki mkubwa sana wa majeruhi. Licha ya kuwa na kiwango bora kabisa na kucheza zaidi ya miaka 18 kwenye ngazi za ushindani akiwa na timu tatu tofauti, lakini mwamba huyu medali ya ligi kwake imekuwa ni kitendawili.
 
3. Pierre-Emerick AubameyangUmri: Miaka 30Klabu alizochezea: Saint-Etienne, Borussia Dortmund, ArsenalMechi za Ligi: 373Amekulia katika akademi ya AC Millan, ambapo baada ya kupandishwa timu ya wakubwa hakuwa anapata nafasi kabla ya kutolewa kwa mkopo Saint-Etienne na baadaye akauzwa Borusia Dortmund mwaka 2011, ambapo alionyesha kiwango bora na baadaye akachukuliwa na Arsenal. Licha ya kucheza kwa mafanikio katika klabu zote alizopita kwenye taji la ligi limekuwa ndoto.
 
5. Juan Matamiaka: 31Klabu alizochezea: Real Madrid, Valencia, Chelsea, Manchester UnitedMichezo ya Ligi: 39Huyu jamaa alikulia Real Madrid, kabla ya kucheza kwa mafanikio katika klabu za Valencia, Chelsea na sasa Manchester United. Katika maisha ya soka la ushindani katika timu ya taifa ya Hispania na ngazi ya klabu ameshinda mataji kibao likiwemo la Ligi ya Mabingwa, Kombe la FA, Kombe la Ligi, Kombe la Dunia la Klabu, Kombe la Dunia, Kombe la Mabara na michuano ya Euro, lakini medali ambayo ameikosa ni ya ligi tu.
 
4. Hugo LlorisMiaka: 33Klabu alizochezea: Nice, Lyon, Tottenham HotspurMechi za Ligi: 470Jina lake ni kubwa sana Ufaransa, hii inatokana na mafanikio aliyopata akiwa na kikosi cha timu ya Taifa ya Ufaransa ambayo ni nahodha. Mwaka 2018 aliiongoza timu hiyo kutwaa Kombe la Dunia nchini Urusi, lakini licha ya kuwa na mafanikio makubwa katika soka la kimataifa, ngazi ya klabu huyu jamaa hajawahi kabisa kutwaa taji la ligi kuu katika klabu zote alizopita.
 
6. Marek Hamsikmiaka: 32Klabu alizochezea : Slovan Bratislava, Brescia, Napoli, Dalian YifangMechi za ligi: 501Huyu ni kiungo wa kimataifa wa Slovenia aliyewahi kucheza na mastaa kibao Napoli - Edinson Cavan na Gonzalo Higuain ambao wote kwa nyakati tofauti wamewahi kubeba taji la ligi hajawahi kutwaa ubingwa wa ligi katika nchi zote alizopita. Kwa sasa Hamsik yuko China huko lakini bado ligi kwake ni ndoto.
 
7. Dimitri PayetMiaka: 32Klabu alizochezea : AS Excelsior, Nantes, Saint-Etienne, Lille, Marseille, West HamMechi za Ligi: 452Kiungo huyu aliyewahi kupita na vilabu kadhaa vya Ufaransa na England, hajawahi kabisa kuchukua ubingwa wa Ligi yeyote licha ya kuwa ana kiwango bora sana, lakini Klabu alizopita ndiyo changamoto kwake kutwaa taji la ligi. Kwa sasa anakipiga kwenye kikosi cha Marseille nchini Ufaransa.
 
8. Laurent KoscielnyMiaka: 33Timu alizochezea: Guingamp, Tours, Lorient, Arsenal, BordeauxMechi za Ligi: 391Mzaliwa wa Tulle, Ufaransa ambaye kwa sasa ameamua kurudi nchini kwao baada ya kucheza kwa miaka tisa Arsenal bila ya kupata taji la Ligi Kuu.Ndoto ya kuchukua kombe ni kama inaenda kufa kwani kwa sasa umri wake umeanza kumtupa mkono hata Klabu anayochezea sasa si kubwa.
 
Back
Top Bottom