Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ukitaka kuizunguka dunia: Ukaenda kaskazini, baadae utajikuta umeanza kurudi kusini, ukifika mwisho wa kusini utaanza kwenda kaskazini tena. Lakini ukitaka kuzunguka kwa kwenda mashariki utajikuta unaenda mashariki tu hadi unarudi ulipokuwa. Jaribisha hili kwenye tufe au chungwa linalozunguka mfano wa dunia.
 
Nchini Marekani, timu za mpira wa miguu za wanawake zinaingiza mapato mengi zaidi ukilinganisha na timu za wanaume. Katika miaka mitatu iliyopita, wanawake wameingiza mapato ya viingilio dola milioni 50.8 wakati wanaume wameingiza dola milioni 49.9. Hata hivyo wanaume wanalipwa mishahara mikubwa zaidi ya wanawake. Wanawake wastani = $4950 kwa mechi Wanaume wastani = $13166 kwa mechi. (CNBC & WSJ)
 
Karibia nchi 40 duniani idadi yake ya watu inapungua kila mwaka. Watu wanaozaliwa ni wachache kuliko wanaokufa, wanaohama ni wengi kuliko wanaohamia. Ujerumani, Japan, Urusi ni moja ya nchi kubwa ambazo watu wake wanapungua.Tanzania ni nchi ya 11 kwa ongezeko kubwa la watu kila mwaka. Kila mwaka 2.75% ya watu wanaongezeka.(IndexMundi)
 
Tafiti: Wanaume wanaowasaidia Wake/Wachumba zao kazi mbalimbali za nyumbani huwa na furaha zaidi na pia tendo la ndoa hufanyika zaidi.
tapatalk_1530901546172.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom