Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

8. Edin Dzeko

Nafasi alizokosa: 16

AS Roma

Katika nafasi 28 alizopata msimu huu kwenye Ligi Kuu Italia, Dzeko amefunga mabao 12 na kukosa mabao ya wazi 16. Staa huyo wa zamani wa Manchester City amekosa zaidi ya nusu ya nafasi alizopata, lakini kamwe huwezi kukuta jina lake likitajwa pale orodha ya majina ya mastraika vimeo inapotajwa, ila yote kwa yote ni mshambuliaji bora kwa sasa Ulaya.
 
7. Chris Wood

Nafasi alizokosa: 17

Burnley

Inawezekana ndiye mchezaji mwenye jina la kawaida kwenye orodha hii akiwa na kikosi cha Burnley msimu huu amefunga jumla ya mabao 11 kwenye Ligi Kuu England. Unaweza kufurahishwa na idadi hiyo ya mabao hasa kulingana na timu anayochezea, lakini ukipata takwimu za nafasi za wazi alizokosa unaweza kushangaa, jamaa kakosa nafasi 17 msimu huu.
 
6. Tammy Abraham

Nafasi alizokosa: 17

Chelsea

Kocha wa Chelsea, Frank Lampard anamkubali kinoma yaani na ndiye straika chaguo la kwanza pale Stamford Bridge akiwaweka benchi kina Olivier Giroud, msimu huu amefunga mabao 13 ya Ligi Kuu England kabla ya kupata majeruhi, lakini amekosa pia nafasi za wazi 17 katika michuano hiyo.
 
5. Gabriel Jesus

Nafasi alizokosa: 18

Manchester City

Pep Guardiola amekuwa akimtumia kama mbadala wa Sergio Aguero msimu huu pale Manchester City na straika huyo amekuwa hafanyi makosa anapopata nafasi ya kucheza, msimu huu amefunga mabao 10 kwenye Ligi Kuu England, lakini pia amekosa nafasi za wazi 18 kwenye ligi hiyo.
 
4. Alvaro Morata

Nafasi alizokosa: 18

Atletico Madrid

Bao lake kwenye pambano la Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora dhidi ya Liverpool ndilo lilimaliza mechi ile ambayo Atletico ilishinda kwa mabao 3-2, lakini ukiacha ushujaa wake huo, kwenye La Liga, Morata amefunga mabao manane tu katika nafasi 26 alizopata, hii inamaanisha kuwa amekosa nafasi 18 za wazi msimu huu.
 
3. Robert Firmino

Nafasi alizokosa: 19

Liverpool

Huyu anatajwa kama kiunganishi cha ule utatu wa Liverpool ambao yupo na Mohamed Salah na Sadio Mane, na kwa kiasi kikubwa Firmino amekuwa mmoja kati ya wachezaji ambao wamekufunga mabao muhimu katika kikosi cha Jurgen Klopp, lakini mbali na kufunga, pia katika nafasi 27 za wazi alizopata msimu huu amezitumia nane tu akifunga huku akikosa nafasi 19 za kufunga.
 
2. Kylian Mbappe

Nafasi alizokosa: 19

Paris Saint Germain

Huyu ndiye mchezaji mwenye thamani kubwa zaidi duniani akikadiriwa kuwa na thamani ya Pauni 227 milioni, na ndiye anaongoza kwa ufungaji Ufaransa akiwa amefunga mabao 18 kwenye Ligue 1 msimu huu, lakini pia Mbappe ni mchezaji ambaye ana rekodi ya kukosa nafasi nyingi kwenye Ligi Kuu Ufaransa akikosa nafasi 19 msimu huu pekee.
 
Eat More by Joe C.
Eat more fruit, the slogans say,
More fish, more beef, more bread!
But I’m on Unemployment pay
My third year now, and wed.

And so I wonder when I’ll see
The slogan when I pass,
The only one that would suit me,
Eat More Bloody Grass!
#Flashback
#IssaTBT
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…