Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Pombe unapokunywa huingia moja moja kwenye damu kwa matumizi ya mwili ndiyo maana unapata matokeo yake kwa haraka. Maji unapokunywa hupitia mchakato wote wa mmeng'enyo (Kufyonzwa) kwaajili ya matumizi katika mwili.
 
Mwaka 2012 Choi Gap Bok alitoroka gerezani kwa kupitia katika tundu la kupitishia chakula kwa wafungwa. Tundu lilikuwa na urefu wa 5.9 inch na upana 17.7 inch. Choi' alikuwa ni mzoefu wa kufanya Yoga, alijipaka mafuta kisha kuanza kujikunja mpaka kupita. Wakati anafanya hayo walinzi walikuwa wamepitiwa na usingizi.
 
Jua huwa linatoa cheche ambazo muda mwingine huwa zinafika karibu na anga la dunia. Mara ya mwisho cheche ya jua kukaribia duniani ilikuwa tarehe 3 Septemba 2012 ambapo iliikosa duniani kwa karibu sana. Wanasayansi wa anga wanatabiri kuwa kuna cheche nyingine itatokea kufikia mwaka 2022 yenye ukubwa sawa na ile ya 2012.(Wikipedia/SolarFlare)
 
Marie Curie' ndiye mwanamke wa kwanza kushinda tuzo ya amani ya Nobel' na pia ndiye mtu pekee ambae ameshinda tuzo hiyo mara mbili (1903 na 1911) pia ndiye mtu pekee aliyeshinda tuzo hiyo katika vitu viwili tofauti (Kemia na Fizikia) hakuna mtu mwingine yoyote mpaka sasa aliyefanya hivyo. Pia ndiye mwanamke wa kwanza kuwa Profesa katika Chuo Kikuu Cha Paris.
 
Jua linatazamiwa kufa kabisa baada ya miaka Bilioni 7-8 ijayo. Mfano kama litakufa kwa wakati huu, itatuchukua dakika 8 kuweza kugundua mabadiliko kadhaa. Baada ya hapo maisha kwa wanyama na mimea kadhaa haitakuwepo japo inakadiriwa baadhi ya mimea itaweza kudumu kwa muda. Baada ya miaka milioni 5 itamezwa kabisa.
 
Elon Musk' ana mpango wa kuleta huduma ya intaneti kwa unafuu zaidi. Mtumiaji utapata GB 300 pamoja na kupiga simu na kutuma meseji bure kwenda eneo lolote Duniani kwa sh 22,000 tu. Wastani wa kawaida GB 300 kupata itakubidi uwe na 300,000 Tsh. Usisahau mpango wake wa kupeleka watu kutalii sayari ya Mars' kuanzia mwaka 2020 unakuja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…