Brazilian Wandering Spider" ni Buibui wanaotajwa kuwa na sumu kali sana. Kwa mwanaume Akikung'ata ukiachana na maumivu makali, Pia Uume' husimama kwa masaa kadhaa bila hiari yako'
Fisi wana kiwango kikubwa cha Asidi katika matumbo yao. Na hiyo ndiyo sababu wana uwezo mkubwa wa kula mizoga' sababu asidi husaidia katika kuua wadudu hatarishi wote wanaopatikana katika mizoga.
Hifadhi ya Taifa Kitulo' inapatikana mpakani mwa Njombe na Mbeya. Moja ya Sifa zake za kipekee ni Bustani ya Mungu' ambapo kuna maua mengi tofauti huku jamii 30 ya maua hayo tofauti huipati sehemu nyingine yoyote Duniani
Ziwa Natroni' linapatikana Arusha. Mojawapo ya sifa yake ya Kipekee ni Kugeuza viumbe kuwa kama Jiwe' pale wanapogusa maji hayo sababu ya kiasi kikubwa cha Chumvi na joto.
NASA wana mpango mpaka kufikia mwaka 2030 kutoka sasa wawe wamefanikiwa kupeleka watu katika sayari ya Mars. Tajiri Elon Musk' yeye anasema atapeleka watu kutalii mwaka 2022 na atajenga nyumba katika sayari hiyo ambayo watu watafikia. Katika safari hiyo, Nauli yake itaanzia Milioni 200 Mpaka Bilioni 1' Tsh.
Ziwa Kisiba linapatikana Mbeya. inasemekana katikati Ya ziwa hilo kuna mali nyingi Za thamani zilizoachwa na Wajerumani kipindi wakiwa wanaondoshwa, Lakini Huwezi kuzichukua sababu Ya mauza uza kibao. Watu husema kuna nyoka mkubwa mwenye vichwa viwili analinda Mali Hizo.
Chura Dume ndiyo hupiga kelele (Sauti) mara kwa mara hususani usiku. Lengo kuu la kelele hizo ni kuvutia majike. Jike akisikia sauti hizo huchagua sauti ipi ya dume katika Jamii yake ambayo ina mvuto zaidi kisha humfuata dume huyo.
Nchini Brunei Wananchi hawalipi kodi kabisa. Ukikamatwa unaiba Unakatwa mikono, Ukikutwa unazini Na unajihusisha na Ushoga Unapigwa na mawe mpaka kufa. Uki Oa Tu unapewa gari
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.