Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Angelina Jolie alikodi mtu wa kumuua baada ya kuzidiwa na msongo wa mawazo. Muuaji huyo alikubali lakini akamwambia asubiri kwa mwezi ndo atamuua. Lengo la muuaji lilikuwa kumpa muda Angelina Jolie abadilishe mawazo, alifanikiwa. (IMDbNews)
 
2011, bibi mmoja nchini Georgia alikata waya wa mkongo wa intaneti unaosambaza mtandao wa intaneti nchini Armenia kutoka Georgia, kukatwa kwa waya huo kulipelekea kukatika kwa intaneti nchini Armenia kwa siku nzima. Alipokamatwa, alidai alikuwa anatafuta scraper za copper ili akauze.(The Guardian)
 
Koh-I-Noor; ndiyo almasi yenye thamani kubwa zaidi duniani. Ina uzito wa karati 105 (21.6 gm). Ipo kwenye taji la malkia wa Uingereza. Hata hivyo siyo almasi kubwa zaidi kuliko zote.Bei yake: Haina bei (priceless)(Most Expensive Diamonds)
 
Othello's Syndrome' ni aina ya ugonjwa wa kisaikolojia ambao unawapata sana wanaume. Mgonjwa anakuwa ma wivu' uliopitiliza kwa mwenza wake. Mtu mwenye ugonjwa huo huamini mwenza wake kuwa sio muaminifu katika mapenzi japo hana ushahidi wowote.
 
Apple' walikuwa katika mpango wa kutengeneza Tablet ambazo ndiyo iPad' kwa sasa. Kilichotokea ni kuwa, Engineers wa Apple wakiwa katika mchakato mzima wa kuandaa Tablet (iPad) walimletea Sampo Steve Jobs ya namna Tablet zitavyokuwa ikiwa na Teknolojia ya Multitourch'.-Steve aliona Sampo hiyo inaweza kufanya kazi pia kwenye Simu alichowaambia Engineers' hao kuwa "Ondoeni Huo Mpango Tablet Tunakwenda Kufanyia Mpango Wa Simu Sasa"-Na Hapo Ndipo Iphone ikazaliwa Rasmi June 29 mwaka 2007..Na IPad zikaja kutolewa rasmi April 03, 2010.
 
Hifadhi ya Taifa Kitulo' inapatikana mpakani mwa Njombe na Mbeya. Moja ya Sifa zake za kipekee ni Bustani ya Mungu' ambapo kuna maua mengi tofauti huku jamii 30 ya maua hayo tofauti huipati sehemu nyingine yoyote Duniani
Inapatikana mkoa wa Njombe bhana wanyakyusa naona wameanza kuisogeza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…