Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tafiti: Wanaume mfumo wao wa mwili umeundwa kulala mara moja baada ya tendo la ndoa, Hii hutokana na Mchanganyiko wa homoni kama norepinephrine, serotonin, oxytocin, vasopressin, nitric oxide (NO) na prolactin ambazo hutolewa pindi wanapofikia kileleni ambazo hupoozesha mwili kwa dakika kadhaa
 
Kutumia chaja ambazo si za makampuni ya simu zinaua simu, Usitumie simu yako wakati unaichaji, Usizime simu yako kamwe, Kuchaji simu usiku kucha kutaiua, Subiri hadi chaji iwe chini kabisa au imeisha ndio uchaji," Hayo ni baadhi ya mambo ambayo si ya kweli kuhusu kuchaji simu.
 
Dola Indidis, Mwanasheria kutoka Kenya, Mwaka 2017 Alikata rufaa Katika Mahakama Ya Kimataifa Ya Haki (ICJ) Akiituhumu Nchi Ya Israeli pamoja na Italia Kwa Kusababisha kifo cha "Yesu". Kabla ya hapo mwaka 2007 alifungua Kesi katika Mahakama Kuu Nairobi lakini ilitupiliwa mbali, Mwaka 2013 Akafungua Kesi (ICJ) napo ikatupiliwa mbali, Na Mwaka 2017 Akakata Rufaa Tena. Anasema "Kifo Cha Yesu kilikuwa kinyume na Haki za Kibinadamu pamoja na Matumizi mabaya ya Ofisi Yaliyofanywa na watawala kwa wakati huo". Alikuwa akitumia Biblia kama ushahidi.
 
Kuna vidonge ambavyo vimeundwa kwa mchanganyiko wa Karati' 24 za Dhahabu, ambapo Ukitumia vinakupa uwezo wa kutoa kinyesi ambacho kina mfanano sawa na dhahabu (Unatoa dhahabu 😊). Kidonge kimoja kinauzwa laki 9 za kitanzania.
 
Mama yake Eminem alimshtaki mwanaye akitaka alipwe TZS Bilioni 23 kwa kumdhalilisha mara kwa mara kwenye nyimbo zake. Kesi ilimalizika kwa Eminem kuamuriwa amlipe mama yake TZS Milioni 57.5. TZS Milioni 53.7 alichukua mwanasheria wake na mama, hivyo mama akabaki na Milioni 3.7.
 
Wakati wa kujamiiana Buibui Dume humviringa Buibui jike ili asiweze kutoka sababu ni Jike huwa na kawaida ya kuwala buibui wengine ikiwemo madume hivyo hufanya hivyo ili kuzuia asije kuliwa na tendo kufanyika kistaarabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…