Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Baada ya kuzamia nchini humo walifikia katika mji wa Windsor Ontario, uliopo kusini mwa nchi hiyo, lakini hawakukaa sana kwa kuwa lilikuwa ni eneo ambalo polisi walionekana kila kona, na badala yake wakaamua kutimkia katika jiji la Edmonton.
 
Jicho la maskauti wa Bayern Munich lilimuona na Julai 25, 2018 dau nono lilitangazwa na Alphonso alichukuliwa akivunja rekodi ya usajili ndani ya Ligi Kuu Marekani akisajliwa kwa Dola 13.5 milioni pamoja na bonasi iliyofikia jumla ya Dola 22 milioni.
 
Staa huyo kijana alikuwa kwenye kikosi cha Bayern kilichotwaa ubingwa wa Bundesliga msimu wa 2018/2019. Pia msimu huohuo walifanikiwa kutwaa ubingwa kombe la DFB-Pokal.

Si hivyo tu, pia aliweka rekodi ya kujumuishwa kwemye kikosi bora cha Ligi Kuu ya Marekani (MLS), mwaka 2018, mchezaji bora wa Klabu ya Vancouver Whitecaps FC mwaka 2018 na goli bora la mwaka la kikosi cha Vancouver Whitecaps FC mwaka 2018.
 
Pia anashikilia rekodi kibao katika ngazi ya timu ya taifa ikiwa ni pamoja na tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Canada kwa upande wa timu ya vijana ya U-17 mwaka 2016, tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa michuano ya Concacaf Gold Cup 2017, kiatu cha dhahabu cha mfungaji bora wa Concacaf Gold Cup 2017, kujumuishwa kwenye kikosi bora cha michuano ya Concacaf Gold Cup 2017 pamoja na tuzo ya mchezaji bora wa Canada mwaka 2018.

Kwa sasa Alphonso anakunja mshahara wa Dola 24,360 kwa wiki katika kikosi cha Bayern Munich, huku taarifa mpya zikieleza kuwa huenda akaongezewa mkataba mpya kutokana na kiwango chake kuwakuna mabosi wa timu hiyo.

Alphonso ana mkataba wa miaka mitano na wababe hao wa Munich, lakini taarifa mpya zinaeleza kwamba huenda wakampatia mkataba utakaomfanya kukaa klabuni hapo kwa miaka tisa, huku dau atakalolipwa pia likipanda hadi Dola 70, 000 kwa wiki.

Nje ya soka, Alphonso ni shabiki mkubwa wa Ligi ya mpira wa Kikapu Marekani (NBA) akiwa pia ni shabiki wa mastaa kadhaa wa ligi hiyo. Vilevile anapenda michezo ya tenisi na raga, pamoja na kriketi.
 
Back
Top Bottom