Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwa sasa supastaa wa PSG, Kylian Mbappe ndio habari ya mjini na anaongoza kuwa mchezaji mwenye thamani kubwa sokoni kuwazidi wengine wote. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa hivi karibuni, Mbappe ametajwa kuwa na thamani ya Pauni 188 milioni.
 
Licha ya kuwa, thamani ya mchezaji huangaliwa kwenye mambo mengi ikiwemo umri, mkataba na hata mechi alizocheza pamoja na mataji ambapo, Mbappe ameweka rekodi ya kubeba taji la dunia akiwa bado kinda. Mbali na Mbappe, hii hapa orodha ya wachezaji wanaoshika nafasi kumi bora kwa thamani kwenye soka la dunia kwa sasa.
 
JADON SANCHO

Borussia Dortmund - £113m

Kinda wa Kiingereza ambaye kwa sasa anatesa Borrusia Dortmund, Sancho. Kwa sasa anawindwa na vigogo huko England, ambapo Manchester United, Chelsea na Liverpool zinaitaka huduma yake.

Dortmund inafahamu inaweza kumpoteza staa huyo kwenye dirisha lijalo la usajili, lakini ada yake haiwezi kuwa ya kitoto
 
LIONEL MESSI

Barcelona - £132m

Ukiona mchezaji bora wa dunia anapoteza thamani yake ujue mambo yametibuka huko. Thamani ya Messi kwa sasa imekuwa ndogo kuliko ya Mbappe, Sancho na Griezmann ambao awali walionekena wachezaji wa kawaida tu.
 
KEVIN DE BRUYNE

Man City - £141m

Fundi wa mpira pale Etihad, De Bruyne ambaye ameiwezesha Manchester City kubeba mataji kibao huku akiwa miongoni mwa waliounda kikosi cha Ubelgiji kilichomaliza nafasi ya tatu kwenye fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018.
 
HARRY KANE

Tottenham - £141m

Nahodha wa Timu ya Taifa England, Kane ni miongoni mwa mastaa wenye thamani kubwa ndani ya kumi bora. Kwa sasa yuko nje kwa muda kutokana na kuwa majeruhi huku chama lake, Tottenham ikipambana na hali yake huko England. Imeshatupwa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na haiko kwenye mbio za ubingwa huko England.
 
MOHAMED SALAH

Liverpool - £141m

Huko Ulaya na England wanafahamu shughuli yake, Mo Salah kwa sasa amekuwa lulu akiwindwa na klabu kubwa Ulaya ikiwemo Barcelona na Real Madrid ambazo zimepania kumng’oa pale Anfield. Kasi na uwezo wake zimemfanya kuwa staa mkubwa na sasa thamani yake imezidi kuongezeka kila kukicha.
 
SADIO MANE

Liverpool - £141m

Mashine nyingine ya Reds, ambaye amekuwa mhimili mkubwa kwenye mafanikio ya Liverpool msimu uliopita hadi kubeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, Mane.

Supastaa wa Senegal ambaye msimu huu amefunga mabao 14 na kutoa pasi saba za mabao na kuifanya Liverpool kuwa kileleni kwa tofauti ya alama 25 dhidi ya Man City, ambaye yuko nafasi ya pili.
 
NEYMAR

PSG - £151m

Dirisha la usajili likifunguliwa tu basi jina la Neymar litaingiza watu vitani. Barcelona na Real Madrid zote zinataka kumng’oa pale PSG. Nahodha huyu wa Brazil mwenye kipaji cha soka na uwezo wa kuchezea mpira, anashika nafasi ya tatu kwa kuwa na thamani kubwa sokoni. Hata hivyo, usajili wake kama ataondoka PSG mwishoni mwa msimu basi unaweza kuvunja tena rekodi ya Euro 198 milioni aliyoiweka wakati akihama Barcelona mwaka 2017.
 
RAHEEM STERLING

Man City - £151m

Supastaa wa Kiingereza ambaye kiwango chake kimekuwa bora zaidi kwenye kikosi cha Man City, anakwenda jino kwa jino na Neymar.

Kucheza chini ya Pep Guardiola kumembadili kabisa Raheem na kuingia kwenye anga za wachezaji bora duniani na hivyo, kupandisha thamani yake maradufu.
 
KYLIAN MBAPPE

PSG - £189m

Mbabe mwenyewe a.k.a The Boss anaongoza orodha ya mastaa wa bei mbaya duniani

Wakati Ronaldo na Messi wakitamba Ulaya, Mbappe alikuwa bado kinda akijaza picha za wanasoka hao kwenye kuta za chumba chake huku akiweka dhamira ya kuja kufuata nyayo zao.

Mzaliwa huyo wa Paris, Ufaransa kwa sasa sio amefuata nyayo tu, bali amekuja kuwazidi thamani na sasa ndio mchezaji mwenye thamani kubwa zaidi duniani tena akiwa bado kijana mwenye umri wa miaka 20 tu.
 
Maumivu ya uzazi ni jambo la kawaida wakati wa ujauzito wa mapacha na unahitaji uangalizi wa madaktari kwa haraka.
uliposema unatamani upate mapacha watatu nimekumbuka nyakati zile nafuatilia variety show inayoitwa return of superman.
siku moja song il kook ahjussi alikuwa anasimulia baadhi ya matukio yaliojiri pindi mke wake alipokuwa mjamzito.

song anasema daktari aliwashauri wamtoe tumboni mtoto mmoja ili kulinda afya ya mke wake pamoja na watoto lakini mke wake akalikataa pendekezo la daktari.


sijui na wewe utaweza kuvumilia kama utakumbana na matatizo ili ndoto yako itimie?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] uvumilivu muhimu sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…